Mshambuliaji Mmisri, Mohamed Salah akimrukia Nahodha wake, kiungo Jordan Henderson kushangilia naye baada ya wote kufunga katika ushindi wa 2-1 wa Liverpool dhidi ya Tottenham Hotspur kwenye mchezo wa Ligi Kuu ya England leo Uwanja wa Anfield. |
Henderson alifunga la kwanza
dakika ya 52 na Sakah la pili kwa penalti dakika ya 75, wakati bao
pekee la Spurs limefungwa na Harry Kane sekunde ya 40 na kwa ushindi huo
Liverpool imefikisha pointi 28 katika mchezo wa 10 sasa ikiwazidi
pointi mbili mabingwa watetezi, Manchester City
Wachezaji wa Manchester United wakipongezana kwa ushindi wa
3-1 dhidi ya wenyeji, Norwich City kwenye mchezo wa Ligi Kuu ya England
leo Uwanja wa Carrow Road, mabao ya Scott McTominay dakika ya 21, Marcus
Rashford dakika ya 30 na Anthony Martial dakika ya 73 dhidi ya moja
la Onel Hernandez dakika ya 88. Kikosi cha Ole Gunnar Solskjaer
kingeondoka na ushindi mkubwa zaidi kama si Rashford na Martial kukosa
penalti 29 na 44