Mazungumzo yakiendelea kuelezea msimu wa Mbio za Ngorongoro min Marathon za mwaka huu April 19 wilayani Karatu picha na Ahmed Mahmoud Arusha |
Na Ahmed Mahmoud Arusha
Msimu wa mbio za Ngorongoro mwaka 2020 umezinduliwa ambapo mbio hizo za mwaka huu zimeboreshwa na zinatarajia kupata washiriki zaidi ya 2000.
Akiongea na vyombo vya habari Mratibu wa mbio hizo kutoka Meta Sport,Meta Petro amesema kuwa mbio zitafanyika 19 April mwaka huu wilayani Karatu kuanzia Geti la Ngorongoro hadi uwanja wa mazingira mjini humo.
Alieleza katika mbio hizo maandalizi yameshaanza na zitakuwa na umbali tofauti kuanzia kilometa 5,km 2.5 na Nusu marathon km 21 na zawadi zitatolewa kwa washindi wa Kwanza 10 wanaume na wanawake kwa mbio za kilometa 5 aliwataka wanamichezo kujitokeza kushikiriki mbio hizo.
“Tunapenda kutumia fursa hii kuwakaribisha watanzania wote pamoja na wenzetu wa mataifa mbali mbali na mataifa jirani kuja kujisajili na kushiriki mbio hizo kwa ni za kipekee ni fursa kwa watanzania kutembelea eneo la hifadhi ya Ngorongoro pamoja na hifadhi jirani”
Kwa upande wake kaimu Meneja wa Mamlaka ya hifadhi ya Ngorongoro Joyce Mgaya alisema kuwa Mamlaka hiyo imelenga kuhamasisha utalii wa ndani kupitia mbio hizo za mwaka huu na watakaa na wamiliki wa mahotel kuweza kuwashawishi kutoa punguzo kwa wageni watakaokuja kipindi Cha mbio hizo.
Alisema kuhusu ugonjwa wa Corona alisema kuwa wamewasiliana na wizara ya Afya na watazingatia muongozo wa wizara hiyo ikiwa ni pamoja na kuweka maji ya kunawa wakati wote na kuboresha Usafi wa mazingira wakati wote wa mbio hizo.
Nae Mwenyekiti wa kamati ya mbio hizo Marcel Bituro alisema kuwa mbio za mwaka huu zimeendelea kuboreshwa kwa kuandaa Nyama Choma Festival na pia unaweza kufanya mambo matatu kwa wakati moja ikiwemo kutembelea hifadhi tatu za Tarangire Manyara na Ngorongoro.