.Afisa
tawala Mkuu wa Chuo kikuu cha Sokoine cha Kilimo SUA Bwana Peter
Mwakiluma akitambulisha wageni mbalimbali waliofika kwenye ufungaji wa
michezo hiyo ya Chibunda Cup 2020 kwa niaba ya naibu makamu mkuu wa chuo
utawala na fedha.
Meneja wa benki ya CRDB tawi la SUA bi. Isabela Kitila akitoa salamu za CRDB ambao ndio wadhamini wakuu wa mashindano hayo.
Meneja
wa Benki ya NMB tawi la Wami bwana Harold Lambikile akizungumza neno
kwa wanamichezo na wadau waliofika kwenye ufungaji rasmi wa michuano
hiyo ya Chibubda Cup.
Naibu
makamu mkuu wa Chuo Utawala na fedha Prof. Amandusi Muhairwa akitoa
salamu za Chuo kwa niaba ya Makamu mkuu wa Chuo Prof. Raphael Chibunda
kuhusu michezo hiyo na umuhimuwake kwa wanajumuiya wa SUA.
Mgeni
rasmi kwenye kufunga mashindano hayo ya Wafanyakazi wa SUA Bi. Asteria
Mwang”ombe ambaye ni Afisa Michezo wa Halmashauri ya Manispaa ya
Morogoro akitoa neno kabla ya washiriki na wadau wa michezo hiyo
iliyofanyika kwenye viwanja vya michezo vya SUA kwenye kampasi ya Edward
Moringe.
Mgeni
rasmi kwenye kufunga mashindano hayo ya Wafanyakazi wa SUA Bi. Asteria
Mwang”ombe ambaye ni Afisa Michezo wa Halmashauri ya Manispaa ya
Morogoro akipata maelekezo kwa waamuzi wa mchezo huo wa mpira wa miguu. Mgeni
rasmi kwenye kufunga mashindano hayo ya Wafanyakazi wa SUA Bi. Asteria
Mwang”ombe ambaye ni Afisa Michezo wa Halmashauri ya Manispaa ya
Morogoro akikagua timu za mpira wa miguu zilizoshiriki kwenye kucheza
mechi ya ufungaji katika ya SUA na Don Bosco. Wachezaji
wa mpira wa wavu kati ya timu ya wafanyakazi wa SUA na DON BOSCO
wakichuana vikali kwenye mchezo wa kufunga michuano hiyo.
**************************************
Na; Calvin Edward Gwabara.
Watanzania
wametakiwa kuhakikisha wanatenga muda kwaajili ya kushiriki kwenye
michezo na mazoezi mbalimbali ya mwili ili kuaidia kujenga mwili na
taifa la watu wenye afya watakaoleta maendeleo.
Wito
huo umetolewa na afisa michezo Manispaa ya Morogoro Bi.Asteria
Mwang’ombe kwa niaba ya mkurugenzi wa manispaa hiyo wakati akizungumza
na wanamichezo na wanajumuiya wa SUA, Benki ya CRDB na NMB wakati
akifunga rasmi michezo kwa ya wafanyakazi wa SUA ya Chibunda CUP.
Bi.
Asteria ameupongeza uongozi wa SUA kwa kuamua kuanzisha michezo hiyo
ambayo inawakutanisha wafanyakazi wote wa SUA kwenye michezo 20
mbalimbali na kuipongeza benk ya NMB kwa kuamua kufadhili mashinano hayo
kila mwaka toka kuanza kwake.
‘’
Naupongeza sana uongozi wa SUA kwa kulipatia kipaumbele swala la michezo
kwa wafanyakazi na wanafunzi hasa kwa kuamua kuanzisha idara maalumu
kwaajili ya michezo Chuoni hii ni hatua nzuri kwani itaongeza ufanisi na
ari ya wanajumuiya wa SUA kushiriki kwenye michezo” Alisistiza Bi.
Asteria.
Afisa
michezo huyo ameahidi kutoa ushirikiano wowote utakaohitajika katika
kufanikisha michezo chuoni hapo ikiwemo swala la walimu wamichezo pale
watakapohitajika na kwamba changamoto mbalimbali zilizobainishwa
atazifikisha kwa uongozi wa manispaa ili kuona namna ya kuzitatua.
Akizungumza
kabla ya kumkaribisha Mgeni rasmi kufunga maichezo hiyo Naibu makamu
mkuu wa chou upande wa taaluma Prof. Amandus Muhairwa kwa niaba ya
makamu mkuu wa chou Prof. Rapgael Chibubda amesema michezo hiyo ni
sehemu ya Chuo kupata wanamichezo ambao watakiwakilisha chou kwenye
michezo mbalimbali ndani nan je ya nchi.
Prof.
Muhairwa amesema Uongozi wa chou unathamini sana umuhimu wa michezo
ndio maana imeweka mikakati mbalimbali ya kuboresha viwanja na kununua
vifaa mbalimbali vya michezo kwenye kampasi zake zote ili wafanyakazi na
wanafunzi washiriki vyema michezo.
‘’
Kutokana na idadi kuwa ya wanafunzi na wafanyakazi Chuo kinaendelea na
jitihada za kuongeza viwanja vipya na vya kisasa ili kukidhi mahitaji na
tayari kiwanja kipya cha mchezo wa kikapu cha kisasa Mkoani Morogoro
tumemaliza kukijenga na sasa kinatumika hat ana watu wan je ya Chuo”
Alifafanua Prof. Mhairwa.
Hata
hivyo ametumia nafasi hiyo kuupongeza uongozi wa benki ya NMB kwa
kufadhili mashindano hayo ya wafanyakazi kwa miaka minne mfululizo
lakini akaomba wadau kuwaunga mkono kwa kujitokeza kufadhili mashindano
ya wanafunzi ili ambayo ni mikubwa na yenye mvuto sana.
Kwa
upande wake Muwakilishi wa banki ya CRDB bi. Isabela Kitila ambaye ni
meneja wa tawi la CRDB SUA ameshukuru uongozi wa SUA kwa kuendelea
kuwashirikisha katika michezo hii kwa miaka minne mfululizo kama
wadhamini wakuu na kuahidi kuendelea kudhamini kila mwaka.
Isabela
amesema kuwa michezo hiyo imewafanya wana CRDB na wanajumuiya wa SUA
kuishi kama ndugu na familia kwakuwa michezo imekuwa ikiwaunganisha kwa
njia mbalimbali na kufahamiana ikizingatiwa idadi kubwa ya wafanyakazi
wa SUA waliopo bila michezo isingekuwa rahisi.
“Niwahakikishie
kuwa sisi kama CRDB mlipo tupo na tutaendelea kuwepo katikati yenu
kwenye kushiriki michezo hii na mambo mengine hivyo karibuni sana kwenye
benki yetu muweze kupata huduma pia za kibenki mbalimbali kulingana na
mahitaji yenu maana sisi na nyinyi ni familia moja” Alisistiza Isabela.
Nae
Menejea wa benki ya NMB tawi la wami bwana Harold Lambileki amesema leo
wao ndio mara ya kwanza kushiriki kwenye michezo hiyo hivyo wamekuja
kujifunza kuona kinachofanyika ili na wao waweze kushiriki kikamilifu
kama wadau muhimu wa michezo nchini.
Amesema
Wanamichezo ndio wateja wa huduma za benki ya NMB hivyo watahakikisha
kwenye michezo ijayo nao wanakuwa sehemu ya wadhamini wa michezo hiyo
muhimu ya wafanyakazi lakini pia kwenye michezo mingine ili kusaidia
kuboresha afya na kuimarisha undug una ushirkiano.
Michezo
hiyo ya wafanyakazi wa SUA ilianza miaka minne iliyopita na imekuwa
ikishidanisha wafanyakazi wote kwenye michezo mbalimbali 20 na mwisho wa
michezo hiyuo zawadi mbalimbali zinatolewa ikiwemo vikombe,medali na
fedha taslimu wa washindi