MANGULA ALIA NA AMANI YA TANZANIA

MbungewaJimbo la Manyoni Mashariki Mhe.
Danieli Mtuka aliyenyanyua mikono akitoa ufafanuzi kwa Makamu Mwenyekiti wa Chama Cha
Mapinduzi (CCM), Tanzania Bara, Philipo Japhet Mangula
(mwenyemiwani) wakati alipotembelea kwenye mradi mkubwa washamba la pamoja la
Korosho lenye zaidi ya ekari 12000 eneo la
Masagati Manyoni Mkoani Singida leo kulia kwa Mangula ni Mkuu wa Wilaya ya Manyoni Rahabu
Jackson Mwagisa (pichana John Mapepele)

Makamu Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), Tanzania Bara,
Philipo Japhet Mangula akikagua Mkorosho kwenye mradi mkubwa wa shamba la pamoja la
Korosho lenye zaidi ya ekari 12000 eneo la
Masagati Manyoni Mkoani Singida leo alipokuwa kwenye ziara ya kikazi ya siku saba katika Mkoa wa Singida(Pichana
John Mapepele

      Makamu
Mwenyekitiwa
Chama Cha Mapinduzi (CCM), Tanzania  Bara, Philipo Japhet Mangula
akikata keki maalum ya miaka
43 ya Chama Cha Mapinduzi katika kikao cha
tathmini na majumuisho ya ziara yake ya kikazi ya siku saba mkoani
Singida kwenye ukumbi wa maktaba wilayani Manyoni leo kulia ni
Mwenyekitiwa
CCM Mkoa wa Singida Alhaji Juma kilimba kushoto ni Mwenyekitiwa CCM
Wilaya ya Manyoni Jumanne Mahanda anayefuata Katibu wa
CCM Mkoa wa Singida AlexndrinaKatabi(Pichana John Mapepele)

    Umati
wa wanachama wa CCM  uliohudhuria mkutano
wa
Makamu Mwenyekitiwa
Chama Cha Mapinduzi (CCM), Tanzania Bara, Philipo Japhet Mangula(Picha na John Mapepele)

Apongeza Mkoa wa Singida 

Na John Mapepele

Makamu Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), Tanzania Bara,
Philipo Japhet Mangula  amewataka
watanzania kutochezea  amani  na 
kuyumbishwa na wanasiasia  na
badala yake  waione amani walio nayo kama
mtaji mkubwa wa kuwaletea maendeleo ya kweli kwa kizazi cha sasa na baadaye.

Mangula ameyasema haya leo katika ukumbi wa maktaba Manyoni
wakati alipohitimisha ziara yake ya kikazi ya siku saba kwenye Mkoa wa Singida
ambapo amesema Tanzania  ni miongoni mwa
nchi chache duniani ambayo imebahatika kuwa amani katika kipindi chote kutokana
na kazi nzuri iliyofanywa na Baba wa Taifa Mwalimu Julius Kambarage Nyerere.
Alisema hivyo ni wajibu  wa kila mwananchi
mzalendo  kuilinda kwa kuwa  watu wengi hawapendi kuona Tanzania  ina amani na kupiga maendeleo ya haraka kama
inavyofanya sasa.

“Ndugu zangu hata tukichukulia mfano mdogo tu, katika kipindi
cha miaka 75 ambayo tulitawaliwa na Wajerumani na Waingereza kwenye Wilaya yote
ya Manyoni  hatukuwa hata na Shule mmoja
ya Sekondari lakini  leo tuna zaidi ya
shule 30 katika kipindi kifupi, je hayo siyo maendeleo makubwa ?” alihoji
Mangula

Alisisitiza kuwa mapinduzi 
makubwa  ya kiuchumi
yanayofanywa  na Serikali ya Awamu ya
Tano inayoongozwa na Rais John Pombe Magufuli yanatokana na  msingi 
imara uliojengwa ambao ni amani na kwamba wachafuzi wa kubwa  wa amani dunani kote ni wanasiasa  ambao wamekuwa wakisukumwa na tamaa ya
madaraka ambapo yakitokea  wanaoumia
ni  watoto, wazee na akina mama.

Akitolea mfano wa machafuko ya kisiasa ya Rwanda ya mwaka 1994
alisema akiwa Mkuu wa Mkoa wa Kagera wakati huo,  alishuhudia wimbi kubwa la watoto na akina
mama wakiteseka  na kufa njiani wakati
wakijaribu kukimbia nchi yao  kunuisuru
maisha yao.

“Nilishuhudia  mama akina
mama  wakitanda kanga na kumsaidia mama
mwenzao kujifungua mtoto pembeni mwa barabara na baada ya kujifungua tu
wakaendelea na  safari, kwa kweli  huwa sipendi kukumbuka  hali ile maana  ni 
hatari na ukatili usioelezeka” aliongeza Mangula

Akiwa katika mkutano huo
amesisitiza suala la uadilifu na kuzingatia sheria,kanuni na taratibu za
chama   cha Mapinduzi ambapo amesema
vitendo vyoyote vya rushwa na wagombea kuanza kujipitisha kabla ya kipindi
rasmi cha kuchukua fomu za kugombea na kuanza mchakato wa uchaguzi hakikubaliki
na kusisitiza kuwa chama kitachukua hatua kwa wote watakao bainika kufanya
hivyo.

Aidha Kamati za Siasa katika maeneo husika zitakazoshindwa
kuwachukulia hatua wanachama watakaofanya makosa zitaadhibiwa.

Akiwa katika ziara hiyo ametembelea  miradi mbalimbali inayotekelezwa na Serikali
ya Mkoa wa Singida ambapo mradi wa mwisho alioutembelea ni mradi mkubwa wa
shamba la pamoja la Korosho lenye ukubwa wa zaidi ya ekari 12000 eneo la
Masagati kwenye Wilaya ya Manyoni na kusifu juhudi zinazofanywa na Serikali
katika kuleta mapinduzi makubwa  ya
kilimo kwa wananchi bila kujali itikadi ya vyama vyao.

Amesema alama ya Chama Cha Mapinduzi ni jembe na nyundo ambapo
amesema jembe ni alama ya mkulima  na
nyundo ni mfanyakazi hivyo CCM inaamini kuwa 
wakulima  na wafanyakazi
wanamchango mkubwa katika kuchangia uchumi wa nchi yao na kuwa   mapinduzi ya uchumi hapa Tanzania yameletwa
na kilimo.

Naye Mbunge wa Jimbo la Manyoni Mashariki Mhe. Danieli Mtuka
akimwelezea Mangula kwenye shamba  la
Korosho la Masagati ameshukuru Serikali ya Mkoa wa Singida chini ya Mkuu wa
Mkoa, Dkt. Rehema Nchimbi kwa kushirikisha wananchi katika  kuwabadili 
mawazo na mtazamo wa kutafuta maendeleo ya kweli  kwa kulima shamba la pamoja la korosho ambapo
amesema wamefanikiwa kwa kiwango kikubwa.

Mhe. Mtuka amesema kutokana na utafiti uliofanyika  na watafiti wa kilimo kutoka Taasisi ya
Utafiti wa Mazao ya Kilimo Naliendele kwa kushirikiana na watafiti wa mazao ya
Kilimo Kanda ya Kati uliofanyika  kuanzia
mwaka  2002, matokeo ya utafiti huo
yalionyesha  kuwa hali ya hewa na udongo
vinafaa kwa kilimo cha korosho hivyo wakaanza kuwahamashisha wananchi kulima
zao hilo

“ Kwa kushirikiana na Uongozi wa Mkoa na Halmashauri tuliamua
kuanzisha zao la korosho kimkakati ili kuchochea kwa kasi kubwa  ukuaji wa uchumi wa mtu mmoja mmoja
wilaya,mkoa  na taifa kwa ujumla’”
aliongeza Mhe. Mtuka

Aidha,alipongeza  Serikali
ya Mkoa kwa kubuni wazo la kuanzishwa kituo kwa kikubwa cha  hija duniani cha Bikira Maria  katika eneo la Sukamahela, sehemu ambayo ni
katikati ya nchi ya Tanzania  kwa ajili
ya watu kutoka sehemu mbalimbali duniani kuja kuhiji.

Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Manyoni Charles
Fussi amesema kuwa kazi  zinazoendelea
katika eneo hilo kwa sasa  ni  kuhamasisha wakulima  wajiunge na kilimo cha korosho, kuendelea
kutoa huduma za ugani kwa wakulima ikiwa ni pamoja na  matumizi sahihi ya viuatilifu kwa
kushirikiana na TARI na Bodi ya Korosho, kuendelea kazi ya kusafisha na kugawa
mashamba kwa wakulima na kuzalisha miche 
bora  korosho.

Kwa upande wake Mkuu wa Wilaya ya Manyoni Rahabu Jackson
Mwagisa  amemhakikishia Mangula kuwa
serikali itaendelea  kusimamia
kikamilifu  na kuwa hamasisha wananchi
kutoka sehemu mbali mbali nchini  kuja
kuwekeza katika  kilimo  cha korosho kwenye eneo hilo kwa kuwa mradi
huo na manufaa makubwa kwa wananchi wa wilaya 
ya Manyoni na Taifa kwa ujumla.

Ametaja baadhi ya manufaa ya mradi huo kuwa ni pamoja na  udhibiti wa 
visumbufu kama magonjwa na wadudu,udhibiti wa  ubora wa korosho kutokana na usimamizi wa
karibu, upatikanaji wa uhakika wa soko katika eneo la mradi,kurahisisha
upatikanaji wa pembejeo na huduma za ugani ili kuhudumia eneo kubwa kwa wakati
mmoja na chanzo kikuu  cha malighafi za
viwanda vya kusindika korosho.

Manufaa mengine ya mradi ni kuongezeka kwa mapato ya Halmashauri
kupitia ushuru na kodi za biashara mbalimbali zitokanazo na ongezeko la uchumi
katika sekta mtambuka zinazoendana na zao hilo, hali ya maisha  kuboreka ikiwa ni  pamoja na ujenzi wa makazi bora na
kuongezeka  uhakika  wa chakula 
katika kaya.