Mbunge venanve mwamoto aangushwa kilolo

DSC_0284
                                                                      Justine Nyamoga aliyeongoza  kura  za maoni
             Na MatukiodaimaBlog

KADA 
wa  chama  cha mapinduzi (CCM) Justine Lazaro Nyamoga  ameibuka na
ushindi wa  kishindo  katika  kura za maoni ndani  ya CCM  jimbo la
Kilolo baada ya kupata  kura 209 kati ya  kura 47  alizopata  aliyekuwa 
mbunge wa  Kilolo aliyemaliza muda wake Venance Mwamoto.

Katika 
matokeo hayo ya kura za maoni yaliyotangazwa majira ya saa nane  usiku 
pamoja na Nyamoga kuongoza kwa kura kada wa  CCM aliyehamia  kutoka
Chadema Brison Kikoti  ameweza  kushika nafasi ya  pili  kwa  wingi wa
kura kwa  kupata  kura 180  wakati aliyepokelewa  ubunge  na Mwamota
Prof Peter Msolla akishika nafasi ya tatu kwa kupata kura 58 sanjari na 
Festo  Kipate aliyepata kura 58  wakati  Mtatifikolo Paulo akipata 
kura 55 .
DSC_0214
                                                 Venance Mwamoto aliyekuwa  mbunge wa  Kilolo

Wengine   
ni pamoja na Danford Mbilinyi  aliyepata  kura 35 na Askofu mstaafu  wa
KKKT dayosisi ya  Iringa Dr  Owdenburg Mdegella  akipata  kura
33,Ashiraf  Chusi  ( 19) Elia Upendo (15) Mgabe Kihongosi (15) Sarufu
Islaeli (14), Mofuga Chelestoni(12), Ole (8),Wiston Mdegella (8),Kenero
Marko (7)  na  wengine  ambao  walipata kati ya 5 na 1  hakuna
aliyepata  ziro katika mchakato  huo ulioshirikisha  wagombea 37

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *