WANANCHI wametakiwa kuhudhuria kwenye mikutano mbalimbali ya kampeni za kugombea nafasi za kisiasa kuelekea kilele cha uchaguzi Mkuu Oktoba mwaka huu ili waweze kuwapima wagombea kwa sera zao.
Hayo na yameelezwa na mgombea ubunge jimbo la arumeru magharibi, Gibson ole Meseiyeki wakati akiongea na wananchi wa jimbo hilo waliohudhuria ufunguzi wa kampeni za ubunge wa jimbo hilo mapema jana katika ofisi za jimbo hilo
Gibson alisema kuwa kwa sasa wapo baadhi ya wananchi ambao mara nyingi wanalalamikia wagombea kuwa hawajatekeleza ahadi wakati ahadi hizo hazikuadiwa
Alisema kuwa mwananchi anapohudhuria ni raisi sana kuweza kunukuu ahadi za mgombea na kisha kuzifuatilia tofauti na pale wanapokaa majumbani
Aliendelea kwa kusema kuwa kwa msimu huu ambao kuna kampeni kila mwananchi anatakiwa kuhudhuria na kutafakari hoja za mgombea
Katika hatua nyingine alisema kuwa yeye kama mgombea ubunge kwa jimbo la Arumeru Magharibi amejipanga kupita kwa wananchi na kisha kuwaeleza kile walichokifanya kwa kipindi cha miaka mitano.
“Kwa kipindi cha miaka 5 iliyopita tumetekeleza miradi mbalimbali ambayo iligusa maisha ya wananchi wa jimbo hili tutaileza kwa kina” aliongeza