Rc makonda awataka wakosoaji wake kuongeza kasi.

  MKUU WA MKOA WA ARUSHA  PAUL CHRISTIAN MAKONDA

NA MATUKIO DAIMA APP, ARUSHA

Mkuu wa Mkoa wa Arusha Mhe. Paul Christian Makonda amesema kamwe hatoacha kuwawajibisha wazembe, wavivu na watendaji wote wa Mkoa wa Arusha wasiotimiza majukumu yao kikamilifu licha ya kuongezeka kwa kelele za ukosoaji unaoelekezwa kwake kutokana na mtindo wake wa Uongozi.


Rc, Makonda ametoa kauli hiyo leo wakati akizungumza na watendaji wa Halmashauri ya wilaya ya Monduli ikiwa ni siku yake ya tatu ya ziara ya kutembelea wilaya zote za Mkoa wa Arusha ili kukagua utekelezaji wa miradi ya maendeleo.

     MAKONDA AKIWASILI WILAYANI MONDULI

Makonda anatoa kauli hiyo kufuatia kutolewa kwa malalamiko yaliyotolewa dhidi yake yakimtuhumu kama mdhalilishaji wa watumishi wa Umma ndani ya Mkoa wa Arusha, hususani wanawake, suala ambalo Mkuu wa Mkoa amelitaja na kusema kuwa halitambabaisha wala kumpunguzia kasi katika kusimamia watendaji wavivu na wazembe wanaoshindwa kutimiza majukumu yao katika kuwatumikia wananchi wa Mkoa wa Arusha.


  MWENYEKITI WA UWT TAIFA MARRY CHATANDA

Itakumbukwa jumamosi ya mei 25 mwenyekiti wa umoja wa
wanawake Taifa (UWT) Marry Chatanda alielezea kusikitishwa na kitendo cha mkuu huyo wa mkoa wa Arusha, Paul Makonda, alichokiita ni unyanyasaji na udhalilishaji wa watendaji wanawake kwenye maeneo yao ya kazi.


Chatanda alitoa kauli hiyo, jijini Dodoma, wakati wa semina ya wabunge wa viti maalum, manaibu waziri, mawaziri, makatibu wa jumuiya ya wazazi ngazi ya mkoa na wilaya ambapo mgeni rasmi alikuwa makamu mwenyekiti wa chama cha mapinduzi (CCM) Tanzania bara, Abdulrahman Kinana, na kusema kuwa kumekuwepo na picha jogefu (Clip) inayozunguka katika mitandao ya kijamii ikionyesha mtendaji wa wilaya ya Longido akiwa anatolewa maneno ya manyanyaso na udalilishaji.


“Kuna Clip imezunguka Kule Arusha, Longido haikuwa jambo jema wala siyo zuri hata kidogo, kama wewe ni kiongozi mkuu wa seikali na umemuona mtendaji wako amekosea ni vizuri ukakaa na kuzungumza nao, kwa suala la udhalilishaji wa wanawake, siwezi kukubaliana nalo tunaomba tuheshimiwe wanawake, tena sisi wanawake ni watendaji wazuri kuliko wanaume” Alisema Chatanda.


   MKURUGENZI MTENDAJI LHRC ANNA HENGA

Kwa upande wake Mkurugenzi wa Mtendaji wa Kituo cha Sheria na Haki za Binadamu (LHRC) Anna Henga  amesema wamepokea kwa masikitiko Video ambayo inaonyesha mkuu wa mkoa wa Arusha akimdalilisha mtumishi ambaye jinsi yake ni ya kike wilayani Longido,na kukemea vikali kauli za udhalilishaji kama hizo.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *