Nbaa na bot yawapiga msasa wahasibu na wakaguzi nchini

Mkurugenzi Mtendaji wa Bodi ya Wahasibu na Wakaguzi wa Hesabu Tanzania (NBAA) CPA. Pius Maneno

Egidia Vedasto

 Arusha.
 Bodi ya Wahasibu na Wakaguzi wa Hesabu Tanzania (NBAA) kwa kushirikiana na Benki Kuu ya Tanzania (BOT) wametoa semina ya mabadiliko ya kidigitali katika huduma za fedha kwa Wahasibu, Wakaguzi wa Hesabu, Mabenka, wanafunzi na watu wengine wanaojighulisha na taaluma hiyo.
Akizungumza na Waandishi wa Habari Jijini Arusha Mkurugenzi Mtendaji wa Bodi ya Wahasibu na Wakaguzi wa Hesabu Tanzania (NBAA) CPA.Pius Maneno amesema semina hii ni muhimu kutokana na mabadiliko ya teknolojia yanayowataka watumishi katika Idara mbalimbali za Fedha kuendana nayo.
Aidha CPA.Maneno ameeleza kuwa, kwa zaidi ya miaka 15 mkutano kama huu umekuwa ukifanyika na kuwapa nafasi watendaji idara za fedha nchini kujadili mambo muhimu yanayohusiana na fedha na mabadilko kidigitali katika utoaji huduma.
“Mkutano huu unatupa nafasi ya kupeana elimu, ujuzi na ufahamu juu ya mabadiliko ya kidigitali, yanayotuwezesha kufanya kazi kwa haraka, kwa muda mfupi na kutoa huduma kwa wateja katika usahihi zaidi”amesema CPA. Maneno. 
Hatahivyo, ametaja mada mbalimbali 11 zitakazojadiliwa katika mkutano huo, baadhi ni pamoja na Mabadiliko ya kidigitali katika utoaji huduma za kifedha za kifedha na taarifa za fedha, Wakaguzi wa ndani na miongozo iliyopo kidigitali, majukumu ya wakaguzi, wahasibu na mabenka katika matumizi ya fedha haramu, Maendeleo endelevu kidigitali katika masoko ya hisa na kutambua fedha zilizotakatishwa.
CPA Maneno ameendelea kutaja mada zingine kuwa ni kuongeza ufanisi katika uwajibikaji kwa maeneo yao ya kazi, changamoto zinazoletwa na matumizi ya kidigitali(zisimuathiri mwekezaji), Kuhusiana na Brella ili Wawekezaji wa ndani waende nje na wa nje waje ndani.
Kwa upande wake Mshiriki wa semina hiyo Mhasibu wa Mradi wa Julius Nyerere (TANESCO) Sarah Mlay amesema semina hii ni muhimu na itawaongezea ujuzi, na ufanisi juu ya mabadiliko na maendeleo ya kidigitali. 
Mhasibu wa mradi wa Julius Nyerere (TANESCO) Sarah Mlay.
“Semina hii inatupa elimu namna ya kupambana na fedha haramu iliyotakatishwa, hii ni namna gani tunatakiwa kwenda kama dunia inavyotaka katika maendeleo na ukuaji wa teknolojia” amesema Mlay. 
Mkutano huo umejumuisha washiriki 700, utakaofanyika kwa siku tatu kuanzia tarehe 29- 31 mwaka huu, kutoka Nchi nzima.
Washiriki wa Bodi ya Wahasibu na Wakaguzi wa Hesabu Tanzania katika semina ya mabadiliko ya kidigitali Jijini Arusha.