Afisa Viwango TBS, Bw.Cyril Kimario
akizungumza na waandishi wa habari katika Ofisi za Makao makuu ya TBS
leo Jijini Dar es Salaam.
********************************
NA EMMANUEL MBATILO, DAR ES SALAAM
Shirika la Viwango Tanzania (TBS)
limeandaa viwango vya Magari yaliyotumika, Spare parts (vipuri) na
gereji, dhumuni la kuandaa viwango hivi ni kuwajengea uwezo wenye gereji
kuendesha shughuli zao kitaalamu ikiwa ni pamoja na kuwaongeza imani
kwa wateja wao ikiwa wamethibitishiwa ubora kwa kiwango husika.
Akizungumza na waandishi wa habari katika Ofisi za Makao makuu ya TBS
Jijini Dar es Salaam Afisa Viwango TBS, Bw.Cyril Kimario amesema magari
yaliyotumika yanakuwa na mifumo ambayo ikitumika kwa muda mrefu
inapoteza ubora wake hivyo inahitajika kufanyiwa marekebisho katika
mifumo hiyo kama vile mifumo ya breki, mifumo ya mafuta, mifumo ya taa,
mifumo ya hewa na mifumo mingine.
“Hiki kiwango cha magari yaliyotumika (used motor vehicles) kimekuwa
kikitumika kwa muda mrefu ambacho ni kiwango namba TZS 698 cha mwaka
2012 ambapo mawakala wetu wa ukaguzi wa magari walikuwa wanakitumia hiki
kiwango kukagua magari kabla hayajaingia nchini”. Amesema Bw.Kimario.
Amesema kuna kiwango kingine ambacho ni kiwango cha Spare parts TZS
1960 ambapo kinapima kwa ujumla vifaa vyote yaani vipuri (spare parts)
ambapo kuna viwango vinavyoambatana navyo kama kiwango cha matairi
specifics, kiwango cha spring specifics, kiwango cha taa specifics, na
kiwango hiki namba TZS1960 ni kiwango cha ujumla kwa vipuri vyote.
“Ili uweze kugundua vipuri hivi (spare parts) vina ubora ni lazima
kiwango hiki kitumike kupima vipuri hivyo (spare parts) na
kikishaangaliwa vizuri na kinaelezea matakwa ya vipuri”. Amesema.
Aidha amesema kuna kiwango kingine cha kupima gereji ambazo
zinarekebisha magari yenye dosari nchini ambacho kimeandaliwa mwaka 2017
hiki kiwango si cha lazima ni kiwango cha hiari ila kinaongeza thamani
pale ambao umekitumia ili kujiridhisha na gereji yako.
“Kiwango hiki kinatoa fursa kwa wamiliki wa gereji kwa ajili ya
kuonesha umahiri wao wa ukarabati wa magari yenye dosari. Kiwango
kinaelekeza namna ambayo gereji inatakiwa kewa na pia vifaa
vinavyohitajika pamoja na mazingira yaweje kulingana na aina ya magari
yanahudumiwa katika gereji hiyo”. Amesema Bw.Kimario.