Rais
wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan amemteua
Prof. Eleuther Alphone Mwangeni kuwa Mwenyekiti wa Bodi ya Uongozi ya
Chuo cha Elimu ya Biashara (CBE) kuanzia tarehe 08 Juni, 2021. Prof.
Mwangeni ni Mhadhiri Mwandamizi wa Chuo Kikuu cha Ardhi (ARU) na
anachukua nafasi ya Prof. Esther Ishengoma ambaye amemaliza muda wake.
Kufuatia
uteuzi wa Mwenyekiti wa Bodi, Waziri wa Viwanda na Biashara, Mhe. Prof.
Kitila Mkumbo , ameteua wajumbe sita (6) wa Bodi hiyo kwa mujibu wa
Sheria ya Chuo cha Elimu ya Biashara ya mwaka 1965 Sura 315 pamoja na
marekebisho yake ya mwaka 2020.
Uteuzi
wa Wajumbe hao utadumu kwa kipindi cha miaka mitatu (3) kuanzia tarehe
09, Juni, 2021. Wajumbe walioteuliwa ni kama ifuatavyo:
1.
Dkt. Consolatha Deogratias Ishebabi ambaye ni Mkurugenzi wa Idara ya
Maendeleo ya Viwanda Vidogo na Biashara Ndogo, Wizara ya Viwanda na
Biashara;
2. Dkt. Kenneth Hosea ambaye ni Mkurugenzi wa Elimu ya Juu, Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia;
3. Bi. Mwema Punzi ambaye ni Wakili wa Serikali Mkuu, Ofisi ya Mwanasheria Mkuu wa Serikali;
4. Bw. Zahoro Muhaji ambaye ni Mjumbe wa Bodi ya Taasisi ya Sekta Binafsi Tanzania (TPSF);
5. CPA. Peter Lucas Mwambuja ambaye ni Rais wa Chama cha Wahasibu Tanzania (TAA);
6. Waziri amemteua Prof. Wineaster Saria Anderson ambaye ni Mhadhiri wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam kuwa Mjumbe wa Bodi ya CBE.