Mwenyekiti wa bodi mpya ya tume ya taifa ya umwagiliaji aweka msisitizo katika kilimo shadidi cha mpunga

 


Mwenyekiti wa Bodi ya Tume ya Taifa ya Umwagiliaji Profesa Henry Mahoo, akizungumza na Menejimenti ya Ofisi hiyo, (haipo pichani) katika makao Makuu ya Ofisi hiyo jijini Dodoma jana jioni.


Kushoto Profesha Henry Mahoo, akimsikiliza Mhaandisi Hassan Dyali alipokuwa akitoa maelezo kuhusu mitambo inayomilikiwa na Tume ya Taifa ya Umwagiliaji.


Picha ikionesha sehemu ya watumishi wa Tume ya Taifa ya Umwagiliaji walipokuwa wakimsiliza Mwenyekiti wa Bodi katika kikao jana jioni.

 

Mwenyekiti
wa Bodi ya Tume ya Taifa ya Umwagiliaji Profesa, Henry Fatael Mahoo,
ameitaka Tume ya Taifa ya  Umwagiliaji kujikita zaidi katika kutoa elimu
kuhusu kilimo shadidi cha mpunga alichoeleza kuwa kinaweza kuongeza
Tija katika sekta hiyo.

Profesa Mahoo, ameyasema hayo Jijini
Dodoma jana Jioni alipokutana na kufanya mazungumzo na Menejimenti na
watumishi wa Tume ya Taifa ya Umwagiliaji.

Alisema kilimo hicho
kinaweza kuleta Tija kwa kuongeza uzalishaji wa Tani saba(7) mpakakumi
(10) kwa hekta katika miradi ya kilimo cha umwagiliaji yenye uhakika wa
maji.

“Tutakuwa tunatekeleza Ilani ya Chama Cha Mapinduzi (CCM)
ya 2020 – 2025 yakufikia malengo yaongezeko la chakula.” Alisisitiza
Profesa.

Sambamba na hilo, Mwenyekiti huyo wa Bodi aliitaka Tume
ya Taifa ya Umwagiliaji kuwajengea uwezo wataalam wake wa ndani pamoja
na wakulima ili kuweza kwenda sambamba na matumizi sahihi ya teknolojia
ya kisasa katika sekta ya kilimo cha Umwagiliji.

Kwa Upande wake
Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa Tume ya Taifa ya Umwagiliaji Bw. Daudi Kaali
amesema kuwa,Tume inaendelea kutekeleza miradi mbalimbali ya Kilimo cha
umwagiliaji nchini ambapo kwasasa imejikita katika kuboresha na kujenga
miradi ya ujenzi shirikishi ambayo haijakamilika.

Aidha aliongeza
kwa kusema kuwa,uzalishaji wa zao la mpunga umeongezeka kwenye maeneo
ya kilimo cha umwagiliaji kutoka tani laki saba na kumi na nneelfu
(714,000) toka mwaka 1989/1990/2000 hadi kufikia tani milioni mbili na
elfu tisa na miambili sabini na nne (2,009,274) mwaka 2018/2019.