Taarifa kwa umma kutoka jeshi la polisi arusha

TAARIFA YA HALI USALAMA KATIKA ZOEZI LA KUJIANDIKISHA DAFTARI LA UCHAGUZI MDOGO WA SERIKALI ZA MITAA. 


Ndugu wanahabari, Hali ya usalama
Mkoa wa Arusha katika zoezi la kujiandikisha kwenye daftari la wapiga
kura uchaguzi mdogo wa Serikali za Mitaa ni shwari mpaka hivi sasa na
hakuna tukio lolote la kihalifu limeripotiwa wala mtu kukamatwa
kuhusiana na zoezi hilo. 


Kwa mujibu wa ratiba zoezi hili
lilikuwa likamilike kesho tarehe 14.10.2019 lakini limeongezewa muda
hadi tarehe 17.10.2019 saa 12 jioni. Jeshi la Polisi mkoani hapa
litaendelea kuimarisha ulinzi na usalama katika maeneo yote ya Mkoa wa
Arusha na litafanya kazi bila kumuonea mtu na halitakuwa na upendeleo
kwa chama chochote cha siasa. Askari wote wameelekezwa kufanya kazi kwa
uadilifu na uzalendo katika zoezi hili. 


Hivyo nitumie fursa hii
kuwahakikishia Wananchi wote wa Mkoa wa Arusha wenye sifa kujitokeza kwa
wingi katika zoezi hili kwani tumejipanga katika kuhakikisha usalama
wao na mali zao. 


Aidha kwa mujibu wa ratiba
tunategemea msimamizi wa uchaguzi kuwasilisha kwa OCD ratiba za mikutano
ya kampeni tarehe 14.11.2019. Kampeni zitaanza rasmi tarehe 17.11.2019
hadi tarehe 23.11.2019. Uchaguzi utakua tarehe 24.11.2019 narudia tena
tarehe za uchaguzi ni zile zile kwa mujibu wa ratiba iliyopangwa na
hazijabadilika. 


Imetolewa na: Jonathan Shanna – ACP Kamanda wa Polisi – Arusha

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *