Katibu
Mkuu Ofisi ya Rais – TAMISEMI, Prof. Riziki Shemdoe (katikati),
akizungumza na Wajumbe wa Menejimenti ya Tume ya Utumishi wa Walimu –
TSC (hawapo pichani), alipotembelea Taasisi hiyo jijini Dodoma Aprili
23, 2021 kujionea utekelezaji wa majukumu. Kushoto kwake ni Naibu Katibu
Mkuu, Ofisi ya Rais – TAMISEMI, anayehusika na masuala ya Elimu, Gerald
Mweli na kulia kwake ni Katibu wa TSC Mwl. Paulina Nkwama.
Katibu
Mkuu Ofisi ya Rais – TAMISEMI, Prof. Riziki Shemdoe (mbele-katikati),
akizungumza na Wajumbe wa Menejimenti ya Tume ya Utumishi wa Walimu
(TSC), alipotembelea Taasisi hiyo jijini Dodoma Aprili 23, 2021 kujionea
utekelezaji wa majukumu. Kushoto kwake ni Naibu Katibu Mkuu, Ofisi ya
Rais – TAMISEMI, anayehusika na masuala ya Elimu, Gerald Mweli na kulia
kwake ni Katibu wa TSC Mwl. Paulina Nkwama.
Naibu
Katibu Mkuu, Ofisi ya Rais – TAMISEMI, anayehusika na masuala ya Elimu,
Gerald Mweli (katikati), akizungumza na watumishi wa Tume ya Utumishi
wa Walimu (TSC), wakati wa ziara ya Katibu Mkuu Ofisi ya Rais –
TAMISEMI, Prof. Riziki Shemdoe (wa pili-kushoto), Aprili 23, 2021 Makao
Makuu ya Tume Dodoma. Wa kwanza kushoto ni Katibu wa TSC, Mwl Paulina
Nkwama.
Katibu
wa Tume ya Utumishi wa Walimu (TSC), Mwl Paulina Nkwama akimkaribisha
Katibu Mkuu Ofisi ya Rais – TAMISEMI, Prof. Riziki Shemdoe (wa
tatu-kushoto) kuzungumza na Wajumbe wa Menejimenti ya Tume hiyo. Prof
Shemdoe alitembelea Makao Makuu ya TSC jijini Dodoma, Aprili 23, 2021
kujionea utekelezaji wa majukumu yao. Kushoto kwa Katibu Mkuu ni Naibu
Katibu Mkuu Ofisi ya Rais – TAMISEMI, anayehusika na masuala ya Elimu,
Gerald Mweli.
Baadhi
ya wafanyakazi wa Tume ya Utumishi wa Walimu (TSC) wakimsikiliza Katibu
Mkuu Ofisi ya Rais – TAMISEMI, Prof. Riziki Shemdoe (wa pili-kushoto)
alipotembelea Makao Makuu ya TSC jijini Dodoma, Aprili 23, 2021 kujionea
utekelezaji wa majukumu yao. Kushoto kwa Katibu Mkuu ni Naibu Katibu
Mkuu Ofisi ya Rais – TAMISEMI, anayehusika na masuala ya Elimu, Gerald
Mweli na wa kwanza kushoto ni Katibu wa TSC, Mwl Paulina Nkwama.
Katibu
wa Tume ya Utumishi wa Walimu (TSC), Mwl Paulina Nkwama (kushoto),
akimkaribisha Katibu Mkuu Ofisi ya Rais – TAMISEMI, Prof. Riziki Shemdoe
(katikati) na Naibu Katibu Mkuu Ofisi ya Rais – TAMISEMI, anayehusika
na masuala ya Elimu, Gerald Mweli (kulia), walipowasili Makao Makuu ya
Tume jijini Ddoma, Aprili 23, 2021 wakiwa katika ziara ya kazi.
Katibu
Mkuu Ofisi ya Rais – TAMISEMI, Prof. Riziki Shemdoe, akisaini Kitabu
cha Wageni, Ofisini kwa Katibu wa Tume ya Utumishi wa Walimu (TSC), Mwl
Paulina Nkwama (wa pili-kulia). Katibu Mkuu alitembelea Makao Makuu ya
Tume jijini Dodoma, Aprili 23, 2021. Wa pili kutoka kushoto ni Naibu
Katibu Mkuu, Ofisi ya Rais – TAMISEMI, anayehusika na masuala ya Elimu,
Gerald Mweli, wa kwanza kushoto ni Mkurugenzi wa Utawala na
Rasilimaliwatu TSC, Moses Chitama na wa kwanza kulia ni Mkurugenzi Idara
ya Ajira, Maadili na Maendeleo ya Walimu TSC, Christina Hape.
Baadhi
ya wafanyakazi wa Tume ya Utumishi wa Walimu (TSC) wakimsikiliza Katibu
Mkuu Ofisi ya Rais – TAMISEMI, Prof. Riziki Shemdoe (hayupo pichani),
aliyekuwa akizungumza nao alipotembelea Makao Makuu ya TSC jijini
Dodoma, Aprili 23, 2021 kujionea utekelezaji wa majukumu yao.
************************
Veronica Simba na Atley Kuni
Katibu
Mkuu Ofisi ya Rais – TAMISEMI, Prof. Riziki Shemdoe, ametoa onyo kwa
watu wanaowatapeli wananchi sehemu mbalimbali kwamba wanahusika kwa
namna moja ama nyingine katika zoezi la kuajiri walimu 6,000 ili kujaza
nafasi zilizoachwa wazi, kama ilivyoagizwa na Rais Samia Suluhu Hassan
hivi karibuni.
Ametoa
onyo hilo leo Aprili 23, 2021 mbele ya waandishi wa habari wakati wa
ziara yake ya kwanza Makao Makuu ya Tume ya Utumishi wa Walimu (TSC)
Dodoma, iliyolenga kujionea utekelezaji wa majukumu yao pamoja na
kuzungumza na watumishi.
Prof.
Shemdoe amewataka watumishi wa umma kuepuka kujihusisha na utapeli huo
kwani wakibainika watachukuliwa hatua kali za kinidhamu na kisheria
ikiwemo kufukuzwa kazi. Aidha, kuhusu vishoka wanaojihusisha na utapeli
huo, Prof. Shemdoe amesisitiza kuwa TAMISEMI itapambana nao vikali.
“Mtumishi
atakayebainika kujiingiza kwenye suala hili la utapeli anaweza kupoteza
kazi. Kwa wale vishoka ambao wameamua kujichukulia fedha za watanzania
wenzetu wakiwahadaa kuwa watawatafutia ajira, tutapambana nao vikali na
tutahakikisha sheria inachukua mkondo wake.”
Kufuatia
hali hiyo, Prof Shemdoe amebainisha kuwa ajira husika zitatolewa kwa
kuzingatia vigezo vitakavyoainishwa katika tangazo litakalotolewa na
Ofisi yake, na kwamba hakutakuwa na upendeleo wa aina yoyote.
“Hakuna
mtu atakayependelewa na hatutaangalia nani katoka wapi. Hizi ni ajira
za watanzania wote, hivyo tutaangalia vigezo ambavyo tutaviainisha
katika tangazo ambalo tutalitoa kwa wananchi na siyo vinginevyo,”
amesisitiza.
Aidha,
amemwagiza Naibu Katibu Mkuu wa Ofisi ya Rais – TAMISEMI, anayehusika
na masuala ya Elimu, Gerald Mweli pamoja na Katibu wa TSC, Mwl Paulina
Nkwama kukaa pamoja na kuunda timu itakayoshughulikia ajira hizo, huku
akisisitiza kuwa timu hiyo iundwe na watu wenye hofu ya Mungu ili
watende haki.
Amesema
Ofisi yake itaendelea kuomba nafasi zaidi za ajira kwani inatambua kuwa
wapo vijana wengi waliohitimu nab ado hawapata ajira.
Katika
hatua nyingine, Katibu Mkuu ameipongeza TSC kwa kazi nzuri inayofanya
hususani katika kusimamia maadili kwa walimu walioko katika utumishi wa
umma. Amewataka watendaji wa Taasisi hiyo kuendelea kutimiza majukumu
yao kwa kuzingatia sheria, kanuni na taratibu hasa wakati wa kufanya
maamuzi katika mashauri ya walimu yanayofikishwa kwao.
“Serikali
imewapa dhamana na imani kubwa kwenu katika kusimamia maadili ya
walimu. Nawaomba muendelee kufanya kazi hiyo kwa imani ileile ambayo
mmepewa.”
Prof
Shemdoe amempongeza Katibu wa TSC, Mwl Paulina Nkwama kwa kuaminiwa na
kuteuliwa na Rais Samia kushika wadhifa huo. Amewataka watumishi wote
kumpa ushirikiano katika kutekeleza majukumu yake.
Akizungumza
katika ziara hiyo, Naibu Katibu Mkuu Mweli, alimweleza Katibu Mkuu kuwa
TSC imekuwa ikifanya kazi nzuri ambapo alibainisha kuwa tangu ashike
nafasi hiyo, Tume imetekeleza kazi walizokubaliana kwa asilimia 90.
Kwa
upande wake, akizungumza kwa niaba ya watumishi wote wa TSC, Katibu wa
Tume Mwl Nkwama alisema kuwa wamefarijika sana kupata heshima ya kuwa
miongoni mwa taasisi za mwanzo zilizo chini ya TAMISEMI, kutembelewa na
Katibu Mkuu ili kujionea utendaji wao.
“Tumefarijika
sana na ujio wako hasa kwa kuzingatia kuwa ni takriban majuma mawili tu
tangu ulipoapishwa na Mhe. Rais kushika wadhifa wa Katibu Mkuu
TAMISEMI. Kwa kuthamini, mchango wa kada ya walimu, umeona ziara yako ya
kwanza ujielekeze kwenye Ofisi ya Tume ambayo ndiyo yenye kushughulikia
masuala mbalimbali ya walimu. Tunaskushukuru sana,” amesema.
Tume ya Utumishi wa Walimu ndiyo Mamlaka ya Ajira na Nidhamu kwa walimu walioko katika utumishi wa umma Tanzania Bara.