Maandamano ya Maadhimisho ya siku ukimwi duniani yakiingia katika viwanja vya soko la kilombero katika Jiji la Arusha 1/12/2020
Meza kuuu mgeni rasmi Kaimu mkuu wa wilaya ya Arusha Nailiba Nyangusi,Kaimu mkurugenzi wa Jiji la Arusha
Kaimu mkuu wa wilaya ya Arusha Nailiba Nyangusi akikata keki kwaajili ya kuchangia vijana wanaoishi na maambukizi ya ukimwi Jijini Arusha katika maadhimisho ya siku ya ukimwi dunia.kushoto kwake ni Diwani wa kata ya levolosi Augustino Mtemu
Dkt.Baraka Mundhe Mratibu wa kuratibu Ukimwi katika Jiji la Arusha akizungumza na waandishi wa habari,juu ya shughuli zilizofanyika katika maadhimisho hayao
Rosemary Tigano Mratibu wa kudhibiti UKIMWI Jiji la Arusha (CHAC)akikata keki katika maadhimisho ya siku ya Ukimwi duniani Jijini Arusha kwaajili ya kuwachangia vijana wanaoishi na Maambukizi ya Ukimwi.
Hanifa Ramadhani Afisa Vijana Jiji la Arusha akizungumza katika maadhimisho ya siku ya ukimwi duniani yaliyofanyika katika soko la kilombero mkoani Arusha
Fatuma Mratibu wa NGO Jijini Arusha akizungumza Katika maadhimisho ya Siku ya Ukimwi duniani
Felista Martini mmoja kati ya WAVIU Akisoma risala mbele ya mgeni rasmi alielezea changamoto mbalimbali wanazopitia ikiwepo baadhi ya Watu wanaoishi na Virusi vya Ukimwi (WAVIU) kuacha kutumia dawa
Kaimu mkuu wa wilaya ya Arusha Nailiba Nyangusi,akimkabidhi kiongozi wa kongamano hilo Arusha kadi za bima ya Afya 120 kulia kwake ni kaimu mkurugenzi Jiji la Arusha Dkt.Kheri Kagya na kushoto kwake ni Diwani mteule wa kata ya Levolosi Augustino Matemu
Felista Martini mmoja kati ya WAVIU Akisoma risala mbele ya mgeni rasmi alielezea changamoto mbalimbali wanazopitia ikiwepo baadhi ya Watu wanaoishi na Vurisi vya Ukimwi (WAVIU) kuacha kutumia dawa
Baadhi ya wakuu wa Idara na vitengo mbalimbali vya Halmashauri ya Jiji la Arusha wakiwa na baadhi ya Viongozi wa Mashirika mbalimbali yasiyo ya kiserikali
Wa kwanza kulia ni Hanifa Ramadhani, Afisa Vijana Jiji la Arusha,katikati ni Mkurugenzi wa Taasisi ya VUKA Initiative ,Rev.Amani Michael
Vijana wakiwa katika mashindano ya kula katika maadhimisho ya siku ya ukimwi duniani katika Soko la Kilombero Jijini Arusha
Vijana kutoka Elimu Yetu wakitoa burudani kwenye maadhimisho ya siku ya Ukimwi duniani katika soko la kilombero lililopo kata ya Levolosi mkoani Arusha
Emmanuel Mgaya a.k.a.Masanja mkandamaizaji akisherehesha katika maadhimisho ya Siku ya Ukimwi duniani Jiji Arusha.
Mmoja wawadau akila keki kwaajili ya kuchangia vijana wanaoishi na maambukizi ya VVU Jijini Arusha.
Pichani ni mabango yakiyobeba kumbe mbalimbali katika maadhimisho ya Siku ya Ukimwi duniani.
Baadhi ya washriki katika siku ya maadhimisho ya ukimwi duniani wakiwa katika viwanja vya sokomla kilombero mkoani Arusha
Na Vero Ignatus,Arusha.
Katika kuadhimisha siku ya ukimwi duniani katika Jiji la Arusha, jamii
imetakiwa kuacha kujihusisha na tabia hatarishi, ikiwemo kushiriki ngono zisizo
salama,ukatili wa kijinsia, ubakaji ,utumiaji wa pombe kupindukia,matumizi ya
dawa za kulevya ,hususanu kujidunga,kwani tabia hizo huchochea ongezeko la
maambukizai mapya ya VVU
Akizungumza mgeni rasmi katika maadhimisho hayo Kaimu mkuu wa wilaya ya
Arusha mjini Nailiba Nyangusi, amesema kuya maambukizi katika
nchi ni asilimia 4.7 kwa Tanzania sawa na asilimia 1.9 katika mkoa wa Arusha
ambapo maambukizi katika jiji la Arusha inaonekana kupungua kutoka asilimia 4.1
mwaka 2015 na kufikia asilimia 2.1 mwaka 2019
Amesema kuwa kundi la vijana lipo kwenye hatari kubwa ya kuambukizwa na baadhi yao hawajitambui, hata hivyo takwimu hizo zinaonyesha kuwa kiwango cha
maambukizi bado kipio juu ukilinganisha na kiwango cha mkoa,hivyo bado kuna
umuhimu wa kuunganisha nguvu za wadau, ili kuongeza kasi dhidi ya mapambano juu
ya maambukizi ya ukimwi
Nyangusi ametoa rai kwa jamii ya jiji lote la Arusha kwa
pamoja ,kushirikiana kuhakikisha wale walio na maambukizi hawapati tena
maambukizi mapya, na wale ambao hawajaambukizwa hawapati maambukizi ,kwa kuwa
hiyo ndiyo maana ya kuoonyesha uwajibukaji ,wa pamoja kama kauli mbiu ya mwaka
huu inavyohamasisha.
Aidha alisema kuwa serikali inaendelea kusimamia
huduma za kuzuia maambukizi kutoka kwa mama kwenda kwa mtoto wakati wa
kujifungua,hivyo imekuwa ikishirikiana na wadau mbalimbali kuendelea kuelimisha
jamii, namna ya kujikinga wasipate maambukizi ya VVU na umuhimu wa kupima ,ili
kama wameambukizwa waweze kuanza dawa kufubaza makali ya vurusi vya ukimwi.
Kwa upande wake Kaimu mkurugenzi wa Jiji
la Arusha Dkt.Kheri Kagya ,alisema kuwa wanapoadhimisha siku ya ukimwi
duaniani, wananchi wanatakiwa kukumbuka kuwa wapo ndani ya siku 16 za kupinga
ukatili wa kijinsia ,iliyoanza tarehe Novemba 25 na kilele chake ni 10/12/2020
ambapo kampeni hiyo hufanyika ikiwa ni utekelezaji wa tamko la haki za binadamu
ikilenga kueneza uelewa wa jamii juu ya jitihada za kutokomeza ukatili wa
wanawake ambapo kauli mbiu isemayo
‘’Tupinge ukatili wa kijinsia :Mabadiliko
yanaanza na mimi
Ikumbukwe ukatili wa kijinsia ni moja
wapo ya kisababishi cha maambukizi ya UKIMWI hivyo jamii inapaswa kuupiga vita
kwa mikakati dhabiti ili iwe salama,pia aliweza kuikumbusha jamii kwamba UKIMWI
bado upo na takwimu zinaonyesha kuwa bara la Afrika hususani kusini mwa jangwa
la Sahara ndio zinaongoza kuwa na kiwango kikubwa cha maambukizi .
Kwa upande wake Dkt.Baraka Mundhe
Mratibu wa kuratibu Ukimwi katika Jiji la Arusha amesema kuwa ratiba ya
maadhimisho yamekwenda kama ilivyofangwa,kwani waliweza kufanya maadhimiso kwa
siku mbili, kwa kuanza upimaji na huduma za uzazi wa mpango, ambapo kilele ni
jana tar 1/12/2020
Amesema kuwa mwitikio kwa wananchi
umekuwa mkubwa kwani wengi wamejitokeza kwa hiyari kupima afya zao na
kujitambua tofauti na ilivyokuwa miaka ya nyuma watu walikuwa wanaogopa
Mwisho.