Jeshi
la Polisi Mkoa wa Mbeya linamshikilia JOYCE KEPHAS AKYOO @ MANKA [31]
Mfanyabiashara na Mkazi wa Stereo Jijini Mbeya kwa tuhuma za kusambaza
taarifa za uongo kuhusu ugonjwa wa Homa Kali ya Mapafu [COVID 19] katika
Mtandao wa Kijamii.

Mtuhumiwa
alikamatwa mnamo tarehe 27.04.2020 majira ya saa 13:30 Mchana baada ya
Jeshi la Polisi Mkoa wa Mbeya kufanya msako huko eneo la Stereo lililopo
Kata ya Manga, Tarafa ya Sisimba, Jijini Mbeya.

Ni
kwamba mnamo tarehe 30.03.2020 majira ya saa 14:09 Mchana mtuhumiwa
alituma taarifa za uongo na zenye lengo la kupotosha kuhusiana na
ugonjwa wa Homa Kali ya Mapafu kwenye kundi “Fans of Mwailubi Car Wash”
katika mtandao wa WhatsApp kwa kuweka picha za marobota ya nguo akieleza
kwa maandishi na kwa sauti baada ya kujirekodi akisema “Mablanket ya
Wagonjwa wa Corona ambao wamefariki nchini China na nguo hizo zinaletwa
barani Afrika na ugonjwa wa Corona” Mtuhumiwa aliendelea kuongea na
kuandika akitahadharisha watu wasikubali msaada huo.

Upelelezi wa shauri hili unaendelea na mara baada ya kukamilika mtuhumiwa atafikishwa mahakamani.
Tangu
kuanza kwa Janga la Homa Kali ya Mapafu [COVID 19] na kutangazwa kama
Janga la Dunia, Serikali kupitia Wizara ya Afya na Viongozi wakuu wa
Nchi ndio wamekuwa wakitoa taarifa kuhusiana na ugonjwa huo pamoja na
namna ya kujikinga dhidi ya maambukizi yake, hata hivyo Serikali imekuwa
ikitoa makatazo mbalimbali kwa wananchi kuacha kutoa taarifa za
kupotosha umma na kusubiri kupata taarifa kutoka vyanzo sahihi.

Aidha
Jeshi la Polisi Mkoa wa Mbeya linaendelea kuimarisha ulinzi katika
maeneo yote ya mpaka wa Tanzania na Malawi, Uwanja wa Ndege wa Kimataifa
wa Songwe, maeneo ya Karantini na kudhibiti magari ya kubeba abiria kwa
kuwataka kupakia abiria kulingana na siti zilizopo [level seat].

Pia
elimu inaendelea kutolewa kwa Wananchi katika maeneo mbalimbali namna
ya kujikinga na ugonjwa wa Homa Kali ya Mapafu unaosababishwa na virusi
vya Corona [COVID 19] na kuwataka wananchi kufuata maelekezo
yanayotolewa na Viongozi Wakuu wa Nchi, Wataalamu na Wizara ya Afya
ikiwemo kuvaa barakoa, kuepuka mikusanyiko, kunawa mikono mara kwa mara
kwa maji tiririka na sabuni au kutumia vitakasa mikono [Sanitizer].

Imetolewa na:
[ULRICH O. MATEI – SACP]
KAMANDA WA POLISI MKOA WA MBEYA.