Mkuu wa mkoa wa Arusha Mrisho Gambo akipata maelezo kutoka kwa viongozi wa JWTZ wakati walipofika kukagua mipaka ya eneo hilo ikiwa ni kujionea na mwisho kutoa maamuzi ya mgogoro huo. |
Wananchi wakiongozwa na Mkuu wa mkoa wa Arusha Mrisho Gambo wakiwa na viongozi wa JWTZ wakikagua maeneo ya wananchi waliovamia eneo la jeshi ambao Jeshi hutumia kwa mazoezi. |
Add caption |
Moja ya nyumba za wakazi eneo la Losirwa kata ya Moshono kama zilivyokutwa na kamera ya matukio jijini Arusha picha zote na Ahmed Mahmoud Arusha. |
Mkuu wa
mkoa wa Arusha Mrisho Gambo amesitisha kwa muda kuendelea na shughuli
yeyote kwenye eneo la Losirwa kata ya Moshono hadi Serikali itakapotoa
maelekezo Mengine ambapo amewaonya Wenyeviti wa Mitaa kuacha kuchukuwa
fedha na kutoa vibali vya Ununuzi wa Ardhi kwenye maeneo yenye Migogoro.
Aidha
Amezitaka halmashauri za wilaya kuacha kutoa vibali vya ujenzi kwa
wananchi kwenye maeneo yenye migogoro kwa kuwa inaleta mikanganyiko
kwenye jamii na kuleta ugumu wakati wa kuitatua.
ametoa kauli hiyo Jana wakati alipotembelea kuona eneo lenye mgogoro
baina ya Jeshi la wananchi wa Tanzania (JWTZ) kikosi Cha 977 kj na
wakazi wa eneo la Losirwa kata ya Moshono jijini Arusha uliodumu kwa
muda mrefu Sasa.
Mara baada ya kukagua eneo hilo na kusikiliza pande zote ametoa maagizo
hayo na kueleza kuwa wananchi waendelee kuwa watulivu hadi Serikali
itakapotoa maelekezo mapya kufuatia mgogoro huo.
kuwa wananchi wengi wanajielewa kama Kuna mtu anaendelea na ujenzi
aaxhie hapo hapo hadi Serikali itakapotoa maelekezo mapya.
tume ya wataalamu kupitia upya na watatoa mapendekezo baada ya taarifa
ndipo tutatoa maamuzi lakini kwa Sasa shughuli zote nimezisitisha”
kuwa Wenyeviti na Tarafa na vijiji wanaopitishia watu vibali vya
kununua Ardhi watawachukulia hatua za kisheria kwani wao ndio chanzo Cha
kuwaingiza wananchi kwenye migogoro.
Upande wao wananchi wa eneo hilo Regina Elias na Poulo Mollel
wakizungumza wameitaka Serikali kuangalia suala hilo kwa kina na kufanya
Tathmini upya kwani wao wameishi muda mrefu eneo hilo na wanategemea
maeneo hayo kwa kujipatia riziki zao za kila siku.
kuwa fedha walizopata kama fidia bado hazilingani na maeneo yao utakuta
mtu amelipwa kiasi kidogo na mwingine amelipwa eneo kama hilo kiasi
kikubwa kwa eneo lenye ukubwa kama huo na Tathmini imekaa muda wa miaka
sita ndipo malipo yamekuja kulipwa bila maandishi yeyote hali inayoleta
mkanganyiko kisheria.
Serikali yetu kwa kuwa sisi tunategemea kilimo na tumeishi muda mrefu
1960 jeshi limenikuta hapa huku jina langu likiwa halipo kwenye orodha
ya malipo naambiwa nikae kifamilia kwani kwenye familia Kuna malipo ya
fidia kwenye eneo langu naomba mkuu wa mkoa tuangalie kwenye suala
hilo”alisema Martha John bibi mwenye miaka 86.