Dc atoa siku saba kwa mhandisi wa jiji la arusha kuweka maji kwenye jengo la kituo cha afya muriet

Mkuu wa wilaya ya Arusha Gabriel Daqarro akiongea mara baada ya kukagua
ujenzi wa madarasa kwenye Shule ya Sekondari Sombetini na kutoa siku
Saba kwa mhandisi kuhakikisha wanaweka maji kwenye kituo Cha Afya huku
akipongeza Ujenzi wa madarasa hayo na kutaka yakamilike kwa wakati picha
zote na Ahmed Mahmoud Arusha.

.Afisa elimu wa halmashauri ya Jiji la Arusha akitoa ufafanuzi mbele ya
mkuu wa wilaya ya Arusha Gabriel Daqarro wakati akipofanya ukaguzi wa
miradi ya maendeleo inayotekelezwa na halmashauri ya Jiji hilo kwenye
Shule ya Sekondari Sombetini picha na Ahmed Mahmoud Arusha.
Mkuu wa wilaya na kamati ya ulinzi na usalama ya Jiji la Arusha
wakikagua madarasa kwenye Shule ya Sekondari Sombetini jijini Arusha
Jana picha na Ahmed Mahmoud Arusha.
Na Ahmed Mahmoud Arusha
Mkuu
wa wilaya  Arusha Gabriel  Daqarro ametoa siku saba kwa kaimu mhandisi 
wa halmashauri ya jiji la Arusha Samwel mshuza    kuweka maji katika
jengo la upasuaji  lililopo katika kituo cha afya  Cha Muriet ili kuanza
shughuli za upasuaji.
Akizungumza
katika siku ya pili ya ziara yake alipotembelea kituo hicho  katika
kukagua ujenzi wa njia yakutembea kwa miguu inayounganisha majengo yote
uliokamilika tarehe 4 March  mwaka huu wenye ghara a ya shilingi milion
100  .
Mkuu huyo amesema
kuwa anatoa siku saba kwa mhandisi huyo kwani maji ni  sehemu kubwa ya
kukwamisha  wananchi kupata huduma ya upasuaji pamoja na shughuli
nyingine ndani ya majengo hayo.
Akiwa
katika shule ya sekondari Taret mkuu huyo  amesema kuwa kabla ya mwaka
wa fedha kuisha  majengo hayo  yawe tamekamilika  ili kuanza mwaka
mwingine wa fedha isiokuwa na Madeni ya nyuma.

Haitaleta maana nzuri kuona tunaanza  mwaka mwingine tukiwa na Madeni
na kutokukamilisha  baadhi ya majengo tunatakiwa kuanza mwaka na miradi
mingine sio ya viporo”. Alisema daqqaro
Hatar
hivyo mkurugenzi wa  jiji  Hilo Maulid Madeni amesema kuwa jiji
limesimamisha shughuli zote za kawaida ili kuweza kukamilisha majengo
yote .
” Mheshimiwa mkuu
wa wilaya tunatambua wewe ni msaidizi wa Rais ndani ya eneo Hilo naomba
nikuahidi jengo hili  ndani yasiku 30 litakuwa limekamilika”.

Akizungumza
mmoja wa wananchi wa eneo Hilo Abdala maguta amesema kuwa wanaishukuru 
serikali  kwa kuendelea kuboresha sekta ya elimu na kuwarahisishia
wanafunzi wengi kutokwenda mashule ya mbali