Uzinduzi wa mradi wa”vuka intiative ” na kampeni ya ”mwogeshe mwanao” wafana arusha

 Mkurugenzi wa Bushback Safari Mustapha Panju akizungumza
katika uzinduzi rasmi wa Mradi wa ”Vuka Initiative” pamoja na
kammpeni ya Mwogeshe Mwanao iliyofanyika katika Hoteli ya Corrido Spring
iliyopo Jijini Arusha
Mwanzilishi wa wa ”Vuka Intitiative” bi Veronica  Ignatus akizungumza katika uzinduzi wa Kampeni ya ”Mwogeshe Mwanao’
 Mkurugenzi wa Taasisi ya Elimu Afrika Daniel Urio akizungumza katika uzimduzi wa mradi wa ”Vuka Initiative” sambamba na Uzindizi wa kampeni ya Muogeshe mwanao
Veila Wilson Mwalimu
wa shule ya msingi Meru mkoani Arusha ambapo ni Mwalimu wa lugha ya
Alama akizungumza katika uziinduzi wa kampeni ya ”Mwogeshe Mwanao”
Mkurugenzi wa Bushback Safari Mustapha Panju akizungumza
katika uzinduzi rasmi wa Mradi wa ”Vuka Initiative” pamoja na
kammpeni ya Mwogeshe Mwanao iliyofanyika katika Hoteli ya Corrido Spring
iliyopo Jijini Arusha
Mtayarishaji wa Keki Elizabeth Membe akisoma maneno yaliyoandikwa kwenye keki hapa (hayaonekeni)
Mwanzilishi
wa Vuka Initiative Bi Veronica Ignatus akikata keki na mmoja wa wageni
Rasmi Mrs Mustafa Panju ishara ya uzinduzi rasmi wa Kampeni ya
”Mwogeshe Mwanao” iliyofanyika Jijini Arusha katika Hoteli ya Corrido
Spring
Keki iliyotumika katika Uzinduzi wa Kampeni ya ”Mwogeshe Mwanao’
Mwanzilishi
wa Vuka Initiative bi Veronica Ignatus akimlisha keki mwanamke mwenye
umri mkubwa (Mama Lily)aliyehudhuria katika uzinduzi wa kampeni ya
Mwogeshe mwanao iliyofanyika Jijini Arusha ikiwa pia ni maadhimisho ya
siku ya wanawake duniani
Mwanzilishi
wa Vuka Initiative bi Veronica Ignatus akimlisha keki msichana mwenye
umri mdogo aliyehudhuria katika uzinduzi wa kampeni ya Mwogeshe mwanao
iliyofanyika Jijini Arusha ikiwa pia ni Maadhimisho ya siku ya  wanawake
duniani.
Shamrashamara
zikiendelea katika uzinduzi wa Kampeni ya Mwogeshe Mwanao katika ukumbi
wa Corrido Spring Hotel iliyopo Jijini Arusha
Shughuli zikiendelea ukumbini kama inavyoonekana
Mwanzilishi wa ”Vuka Initiative” Bi Veronica Ignatus  akiwa na baadhi ya wanawake mara baada ya kufanyika kwa Uzinduzi wa kampeni ya” Mwogeshe Mwanao” iliyofanyika katika hotel ya Corrido Spring Hotel Jijini Arusha
 Mwanzilishi wa  Mradi ”Vuka Initiative”  bi Veronica Ignatus akiwa kayika picha ya pamoja ba baadhi ya viongozi na wageni waalikwa katika uzinduzi wa Kampeni ya ”Mwogeshe Mwanao” 
Na.Mwandishi wetu, Arusha.
Katika
kusheherekea sikukuu ya wanawake duniani 8/3 wazazi na walezi
wametakiwa kujenga uhusiano wa karibu na Watoto wao na kutenga muda
malezi na ufuatiliaji wa karibu mabadiliko ya tabia za watoto.
Hayo yamesemwa na Mkurugenzi wa Bushbuck Safari Mustapha Panju alipokuwa akizindua mradi wa “Vuka Initiative” pamoja na uzinduzi wa kampeni ya  Mwogeshe Mwanao iliyofanyiaka katika Hoteli ya Corrido Spring mkoani Arusha.
Mustapha Panju ameitaka
jamii kubadilika kifikra na kuacha visingizio vya kubanwa na  majukumu
ya kila siku kwa kisingizio cha kupanda kwa haki ya maisha badala yake
watenge muda wa kuwa na watoto wao mara kwa mara kwani watoto wengi
wamewazowea wasaidizi wa majumbani kuliko wazazi wao au walezi wao
halisi
Mwanzilishi wa Mradi wa Vuka Initiative Bi Veronica Ignatus alisema kuwa Vuka Initiative” ni
mradi wenye kusudi la kupunguza changamoto za ukatili na unyanyasaji wa
kijinsia katika jamii. Dira yake ni kuwa taasisi kimbilio kwa watu wote
wenye changamoto za kimaisha.

Pia
alisema kuwa Dhima yake ni kuifikia jamii na kutatua changamoto za
ukaliti na unyanyasaji wa kijinsia ambapo Motto wao unaowaongoza ni “Vuka yako, Salama yako”
Bi Veronica alisema kuwa mradi
huu unatarajia kuanza kufikia watoto na wanawake katika makundi ya
wanawake yaani wafanyakazi wa sekta rasmi na zisizorasmi, mpango ni
kuanzia na wilaya sita za mkoa wa Arusha.
Vuka Initiative umelenga
kwa dhati kuisaidia serikali ya awamu ya tano ya Rais John Pombe
Magufuli ya kuwaboreshea maisha na kuwawezesha wanawake na watoto.
Namna au mbinu ya kuifikia jamii itakuwa kwa kuandaa vipindi, warsha, semina, makongamano ya kuwafikia wanawake na Watoto.
Vuka Initiative itatumia kampeni ya “Mwogeshe Mwanao” kampeni
hii inalenga kuwakumbusha wazazi na jamii kwa ujumla kuhusu jukumu la
kuongeza ukaribu/mahusiano kwa watoto wao na kutenga muda wa malezi na
ufuatiliaji wa karibu kwa Watoto wetu. 
Vuka Initiative inatoa
wito kwa jamii, vyombo vya habari na wadau mbalimbali kuunga mkono
kwenye tukio na kuwa huru wakati wote kutoa ushauri, mapendekezo, maoni
na michango ya hali na mali katika kuwezesha utekelezaji wa majukumu ya
kuitumikia jamii na Taifa kwa ujumla.