Shilingi bilioni 1.5 kujenga chuo cha veta tabora(uyui)

Na Daud Tiganya
Halmashauri
ya Wilaya ya Tabora(Uyui) limeishukuru Serikali kwa kuwapatia kiasi cha
shilingi bilioni 1.5 kwa ajili ya ujenzi wa Chuo cha Ufundi Stadi
(VETA)  cha  kisasa kitakachojengwa  eneo la Isikizya wilayani humo.


Fedha
hizo zitasaidia katika ujenzi wa majengo ya fani mbalimbali iiwemo
ushonaji, ufundi umeme, uhazili na komputya  na uchomeleaji vyuma
(welding)

Kauli
hiyo imetolewa leo na Mwenyekiti wa Halmashauri hiyo Said Ntahondi
katika kikao cha  Baraza la Madiwani wa kupitia taarifa za utekelezaji
wa miradi mbalimbali ya maendeleo.

Alisema
kukamilika kwa Chuo hicho cha VETA kutasaidia vijana ambao wamemaliza
elimu ya Shule za Msingi na Sekondari kusomea kozi mbalimbali ambazo
zitawawezesha kujiajiri wenye kwa ajili ya kuondokana na umaskini.

“Katika
hatua nyingine Mwenyekiti wa Halmashauri hiyo alisema Hospitali ya
Wilaya ya imeanza kufanya kazi kwa kutoa huduma za matibabu ya wagonjwa
wan je.

Alisema
kuwa hatua hiyo imefikia baada ya agizo la Mkuu wa Mkoa wa Tabora la
kumtaka Mganga Mkuu wa Wilaya hiyo kuanza na utoaji wa huduma za awali
katika majengo ambayo yamekamilika ili kuwapunguzia adha za wananchi
kutembea umbali mrefu kutafuta huduma za matibabu.

Alisema
kwamba kuanza utoaji wa huduma kwa Wagonjwa wa Nje(OPD) kumesaidia
kupunguza usumbufu kwa wananachi wa wilaya hiyo kwa kupata huduma za
matibabu kuwa karibu na wananchi.

Wakati
huo huo Ntahondi alisema kuwa Halmashauri hiyo imetenga shilingi
milioni 60 kwa ajili ya ujenzi wa majengo katika Sekondari saba ili
kupunguza mrundikano wa wanafunzi wa Kidato cha kwanza.

Alisema
sanjari na hilo wanaomba Ofisi ya Kanda ya Udhibiti ubora kuwasaidia
ili Shule ya Sekondari ya Idete iweze kupokea wananfunzi wa Kidato cha
Tano mwaka huu.

Ntahondi
alisema wanaendelea na wanaandalizi kwa ajili ya uanzishwaji kwa Kidato
cha Tano kama watakubaliwa ili Wilaya hiyo iweze na Shule za sekondari
za Kidato cha tano na sita mbili ikiwemo ya hivi sasa ya Ndono.