Rais
Magufuli amesema shughuli za kidini ama kiimani, hazipaswi kufungwa
kutokana na maafa ya vifo vya watu 20 mkoani Kilimanjaro,
yaliyosababishwa na watu kukanyagana, wakiwahi kukanyaga mafuta ya
upako, badala yake yashughulikiwe mapungufu yaliyojitokeza.

Mkuu
wa Mkoa wa Kilimanjaro, Anna Mghwira ametoa ujumbe huo wa Rais Magufuli
jana wakati wa mazishi ya kitaifa ya watu 19, kati ya 20, yaliyofanyika
kwenye Viwanja vya Mashujaa mjini Moshi. Watu hao walikufa baada ya
kukanyagana walipokuwa wakifuata mafuta ya upako ya Mtume Boniface
Mwamposa.

“Asubuhi
wakati nazungumza na Rais kuhusu tukio hili, alisisitiza tushughulikie
mapungufu yaliyojitokeza, badala ya kufunga shughuli za kiimani…mimi
nasema tuzingatie vibali vyetu ili kuepusha maafa kama haya,” amesema
Mghwira.

Alisema
tayari Jeshi la Polisi, linafanya uchunguzi kuhusu tukio hilo, ambapo
pia viongozi waandamizi wa Mtume Mwamposa, wanashikiliwa kwa mahojiano
zaidi.

Mghwira
alisema pia baadhi ya watu, wanaodhaniwa ni vibaka, walikuwa miongoni
mwa vyanzo vya watu kupata maafa hayo, kutokana na kitendo cha kujaribu
kuwaibia waumini waliokuwa wakitoka mlangoni.

“Ninyi
vibaka ambao ni sehemu ya maafa haya, lazima mjue damu ya watu
iliyopotea na iliyomwagika, itakuwa juu yenu na malipo yenu yanakuja,”
alisema mkuu wa mkoa.

tukio hilo limegusa pia wananchi wa mikoa ya Arusha, Manyara na
Kilimanjaro. Kwa upande wao, viongozi wa madhehebu ya dini, walisema
wanapinga mfumo wa maombezi ya kidini, unaofanywa sasa kwa kasi, kwa
kigezo cha kuleta uponyaji kwa waumini wao.

Aidha,
viongozi hao waliomba serikali kutazama baadhi ya madhehebu,
yanayotumia mgongo wa dini na ufahamu mdogo wa waumini katika kuwarubuni
na kuwasababishia maafa.