Mtume boniface mwamposa atiwa mbaroni

Waziri
wa Mambo ya Ndani ya Nchi, George Simbachawene amesema wamemkamata
Mtume Boniface Mwamposa Jijini Dar es salaam alipokuwa amekimbilia baada
ya kutoroka mkoani Kilimanjaro kutokana na tukio waumini wake kugombea
kukanyaga mafuta ya upako na kusababisha vifo vya watu 20.



Simbachawene ametoa pole kwa Familia ya Watu 20 waliopoteza maisha wakati wakitoka katika ibada hiyo  Mjini Moshi.

Amesema
Wizara itaweka Kanuni na Taratibu kali za Usajili wa Taasisi zinazotoa
Huduma za Maombezi(Ministries) ambazo baadhi zinavunja Sheria.