Na. Catherine Sungura-Dodoma
Serikali
kupitia Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto
imeahidi kuipatia kiasi cha shilingi bilioni mbili hospitali ya rufaa ya
kanda KCMC ili kuweza kutoa huduma za tiba za mionzi hospitalini hapo.

Hayo
yamesemwa jana na Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na
Watoto Ummy Mwalimu wakati akijibu maswali kwa kamati ya kudumu ya
Bunge ya huduma na maendeleo ya jamii jijini hapo.

“Tumekubaliana
na Katibu Mkuu kuitafuta hiyo bilioni mbili kwa ajili ya ujenzi wa
jengo la mionzi (bunker) kwa hospitali hii tutawapatia”.

Aidha,
Waziri Ummy amesema kuwa wizara yake inayo muelekeo kwa hospitali zote
za rufaa za kanda kutoa huduma za mionzi hivyo hakutakuwa na haja ya
wagonjwa wa kanda ya kaskazini kusafiri hadi Ocean road kupata huduma za
mionzi.

“Wizara
tumeanza kutoa huduma za mionzi,mwaka jana tulizindua hospitali ya
Bugando,lengo letu ni kuweka huduma hizi kwenye hospitali zote za rufaa
za kanda kama Mbeya na tunafikiria kuweka na hapa kwenye hosputali ya
Benjamin Mkapa”.Alisisitiza Waziri Ummy

Hata
hivyo Waziri Ummy amesema wizara imeweza kuwapatia hospitali ya KCMC
fedha kwa ajili ya watumishi pamoja na dawa kiasi cha shilingi bilioni 5
katika kipindi cha miezi sita.”Kama serikali itaendelea kuthamini suala
la ubia katika utoaji wa huduma za afya na mashirika ya dini na watu
binafsi”.

Naye
Mkurugenzi Mtendaji wa KCMC Dkt. Gilliard Masenga amesema kuwa asilimia
sitini ya wagonjwa wa saratani wanahitaji huduma ya mionzi na
hospitali hiyo imeweza kuona jumla ya wagonjwa 4323 kwa kipindi cha
mwaka jana na kufanya uchunguzi wa magonjwa ya saratani ambapo kati yao
watoto 239 na watu wazima ni 4084,aidha wamefanya kampeni maalum ya
upimaji na ushauri katika wilaya ya Arumeru na watu 307 walipatiwa
huduma ya uchunguzi wa awali wa saratani