Wasiojulikana waiba vifaa vya nida wilayani kwa dc muro

Watu
wasiojulikana wameiba mashine zote za Mamlaka ya Vitambulisho vya
Taifa(NIDA) zilizokuwa katika kituo kidogo cha NIDA katika Halmashauri
ya Wilaya ya Arusha, Wilaya ya Arumeru Mkoani Arusha usiku wa kuamkia
leo, kituo hicho kimefungwa kwa leo na Polisi wameanza mchakato wa
kuwasaka waliohusika na wizi huo.

Mkuu
wa wilaya Arumeru, Jerry Muro amesema wizi huo umetokea usiku wa
kuamkia leo Jumatatu Januari 6, 2020 katika ofisi za Nida zilizopo jengo
la halmashauri ya Wilaya ya Arusha (DC).

Muro amesema vifaa vilivyoibwa ni kamera mbili, stendi mbili, kompyuta
mpakato mbili, kompyuta moja (Desk top), stendi mbili, Extation mbili,
keyboad moja na Damalog moja.

“Vifaa
vyote vimeibiwa, tumepata mshtuko, milango haikuvunjwa inaonekana ni
wizi wa kimkakati umefanywa ndani, vifaa vya NIDA ni mali za Taifa sasa
hawa wanapata wapi ujasiri wa kuiba!”- Jerry Muro, Mkuu wa Wilaya
Arumeru