Kagera awaagiza wakurugenzi na wakuu wa wilaya kuhakikisha wanatenga shilingi elfu moja kwa kila mtoto ili kupambana na udumavu

Na Clavery Christian Bukoba Kagera.
Mkuu wa mkoa Kagera
Brig. Jen. Marco E Gaguti amewaagiza wakurugenzi na wakuu wa wilaya
mkoani humo kuhakikisha wanatenga fedha za huduma ya chakula kwa watoto
wadogo kulingana na watoto walioko kwenye halmashauri ikiwa ni lengo la
kupambana na udumavu wa akili kwa watoto unaonekaka kuwa mwingi mkoani
licha ya mkoa huo kuwa kati ya mikoa mitano bora hapa nchini
inayozalisha chakula kingi.

RC
Gaguti amesema kuwa eneo la kwanza ambalo mkoa huo halifanyi vizuri ni
eneo la utoaji fedha kwenye mipango ya halmashauri ambapo amesema kuwa
taarifa aliyoipokea mara ya mwisho halmashauri zote zilikuwa na alama
nyekundu ikiashiria hatari kwa sababu ya kushindwa kutenga fedha na
kuzitoao ambapo kila halmashauri inapaswa kutenga shilingi elfu moja kwa
kila mtoto.

“Moja wapo
ya jambo la kwanza ambalo nataka tuliwekee mikakati na maazimio baada ya
kikao hiki ni kuhakikisha halmashauri zetu zote tunatenga fedha
kulingana na idadi ya watoto tuliyonao ili kuhakikisha tunawanusuru
watanzania hawa, inawezekana leo tukaona maumivu ya fedha kwasabu ya
mipango tuliyonayo au changamoto ya bajeti lakini faida zake ni kubwa
mara miamoja zaidi sababu unafanya ukombozi wa kijana mwenyewe” Amesema
RC Gaguti.

Amesema kuwa
lengo la kuhimizwa kutoa shilingi elfu moja kwa kila mtoto mdogo chini
ya miaka mitatu ni kiweza kumkomboa huyu mtoto ili serikali isiendelee
kumuhudumia maisha yake yote kwasababu ikishindwa kumuhudumia hapa ni
kwamba itaweza kumuhudumia maisha yake yote kitu ambacho itakuwa ni
hasra kwa serikali. Nakiwata viongozi wa idara mbalimbali kutochukulia
swala la lishe kama swala la kawaida.

“Naomba
tusichukulie swala hili kirahisi mtu anasema mboma hafi yawezekana
alisha kufa kama ubongo wake upo chini ya asilimia 50% ni bahati ya
Mungu tu mti huyu anakuwa amekufa” Amesema RC Gaguti.

Kwa
upande wake afisa lishe kutoka TAMISEMI bi Bertha Mwakabage amesema
kuwa changamoto kubwa sana ni kupambana na udumavu kuanzia kwenye
unyonyeshaji ndo maana wanataka mtoto apatiwe vyakula vyenye kuleta
virutubisho kwa kutengeneza ubongo mzuri wa mtoto kwa kunyonya na kula
vyakula vinavyomjenga mtoto akiwa bado mdogo.