Mbunge
wa Kawe Halima Mdee anashikiliwa na Polisi katika kituo cha Oysterbay,
kufuatia agizo la Mahakama ya Kisutu la kukamatwa kwa wabunge wanne wa
CHADEMA.
Jeshi la Polisi Kinondoni limesema Mdee ameripoti mwenyewe kituoni hapo
leo Novemba 16, 2019 na atafikishwa mahakamani siku ya Jumatatu.
‘Ni kweli yupo hapa kituoni tunamshikilia kama ambavyo Mahakama iliagiza
na yeye amekuja mwenyewe kuripoti hapa, hivyo taratibu zote za kipolisi
zinafanyika na Jumatatu atafikishwa mahakami’, amesema Msaidizi wa RPC
Kinondoni.
Amri hiyo ya kukamatwa kwa wabunge hao Halima Mdee, Peter Msigwa, John
Heche na Ester Bulaya, ilitolewa jana, Novemba 15, 2019 na Hakimu Mkazi
Mkuu wa Mahakama hiyo Thomas Simba, ambapo alisema kuwa kesi hiyo
ilifikishwa mahakamani hapo kwa ajili ya upande wa mashtaka kumhoji
Mbowe na baada ya kumaliza kutoa ushahidi wake kutoka upande wa utetezi
na ndipo ilipobainika washtakiwa hao wanne kutokuwepo mahakamani.