Picha ya rais magufuli yamponza idris sultan ….makonda amtaka ajisalimishe polisi

Mkuu
wa Mkoa wa Dar es Salaam Paul Makonda, amemtaka mchekeshaji na
muigizaji hapa nchini, Idris Sultan, kuripoti katika kituo chochote cha
polisi, hii ni baada ya msanii huyo ku ‘post’ picha katika ukurasa wake
wa Instagram, akiwa amehariri picha ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa
Tanzania Dkt John Pombe Magufuli na kuweka sura yake.

Makonda ametoa agizo hilo leo Oktoba 30, 2019, kupitia ukurasa wake wa Instagramu.

“Naona
mipaka ya kazi yako huijui, nenda sasa hivi kituo chochote cha Polisi,
uwaambie Makonda kaniambia nije utakuta ujumbe wako”
ameandika Makonda.

Idris
aliweka picha hizo ikiwa ni siku moja tu imepita tangu Rais Magufuli,
atimize umri wa miaka 60, ambapo msanii huyo aliandika kuwa.

 “Kwa siku moja tukabadilishana kazi ili a-enjoy birthday yake kwa amani”.