Mkuu wa Mkoa wa Tanga Martine Shigella akizungumza wakati wa maadhimisho hayo
Mganga Mkuu wa Mkoa wa Tanga (RMO) Jonathan Budemu akizungumza wakati wa maadhimisho hayo
Mwenyekiti
wa Taifa wa Chama cha Wazazi chenye malengo ya kutoa elimu ya Kichwa na
Mgongo Wazi (ASBAHT) Abdulhakim Bayakub akizungumza wakati wa
maadhimisho hayo kushoto ni Waziri wa Afya Maendeleo ya Jamii Jinsia Wazee na Watoto Ummy Mwalimu na Mbunge wa Viti Maalumu (CCM) Mkoa wa Tanga
Waziri wa Afya Maendeleo ya Jamii Jinsia Wazee na Watoto Ummy Mwalimu na Mbunge wa Viti Maalumu (CCM) Mkoa wa Tanga kushoto akimkabidhi cheti Mfanyakazi wa Benki ya NMB Jeniffer Mtey kwa ajili ya udhamini wa maadhimisho hayo
Waziri wa Afya Maendeleo ya Jamii Jinsia Wazee na Watoto Ummy Mwalimu na Mbunge wa Viti Maalumu (CCM) Mkoa wa Tanga kushoto
akimpongeza mtoto mwenye ulemavu wa kichwa kikubwa Joaly Salehe ambaye
aliimba wimbo wakati wa maadhimisho hayo kushoto ni Mkuu wa Mkoa wa
Tanga Martine Shigella akifuatiliwa na Mkuu wa wilaya ya Kilindi Sauda
Mtondoo
Waziri wa Afya Maendeleo ya Jamii Jinsia Wazee na Watoto Ummy Mwalimu na Mbunge wa Viti Maalumu (CCM) Mkoa wa Tanga akiwa kwenye picha ya pamoja na viongozi mbalimbali
Waziri wa Afya Maendeleo ya Jamii Jinsia Wazee na Watoto Ummy Mwalimu na Mbunge wa Viti Maalumu (CCM) Mkoa wa Tanga katikati akiwa kwenye picha ya pamoja na madaktari
wanaozaliwa kila siku nchini watatu wanazaliwa wakiwa na matatizo ya ulemavu wa
kichwa kikubwa na mgongo wazi idadi ambayo imeelezwa kwa mwaka inafikia watoto
4800.
hizo zilitolewa leo na Waziri wa Afya Maendeleo ya Jamii Jinsia Wazee na Watoto
Ummy Mwalimu wakati wa maadhimisho ya siku ya mtoto wa kichwa kikubwa na mgongo
wazi duniani.
hayo yalifanyika Kitaifa kwenye viwanja wa Tangamano mjini Tanga ambapo alisema
kwamba serikali imekuwa ikiweka juhudi kubwa kuweza kuhakikisha inatokomeza
suala hilo.
kwamba wakati umefika jamii kuacha kuwa na mila potofu kwa watoto wenye vichwa
vikubwa na mgongo wazi na dhana hiyo ianze kwa wazazi, walezi na familia
inayowazunguka.
imani potufu ndio zimepelekea wazazi na walezi wa watoto hao kutumia fedha nyingi
kwa waganga wa kienyeji bila mafaanikio na kusababisha ongezeko la vifo vya
watoto wao”Alisema Waziri Ummy.
aliitaka jamii kutambua kwamba mtoto akizaliwa na kichwa kikubwa sio
laana,mkosi wala balaa huku akiwataka kuachana na imani potufu kwani wameambiwa
na wataalamu chanzo cha watoto kuzaliwa hivyo ni kutokana na upungufu wa madini
ya foliki Acidi na virutubisho muhimu vinavyotokana na kwenye vyakula nyingi
vilivyopo hapa nchini,.
niwaase wakina mama wajawaziti kutumia vitamin hiyo kabla ya kupata ujazito huku
akitoa wito kwa wanawake wenye umri wa kuzaa miaka 15 hadi 49 kuzingatia ulaji
bora wa vyakula vyenye vitamin ya aina ya foliki acidi ikiwemo mbogamboga na
matunda”Alisema Waziri Ummy
alisisitiza umuhimu wa kila mwanamke aliyefikia umri wa kuzaa wajawazito kwenda
kliniki mapema mara wanapogundua ni wajawazito ili waweze kupatiwa huduma za
afya ikiwemo vidonge vyenye vitamini ya foliki acid.
akizungumza kabla ya kumkaribisha mgeni rasmi Mkuu wa Mkoa wa Tanga Martine
Shigella alisema kwamba tatizo hilo linazuilika na kumalizika kabisa kwenye jamii
kwa kutoa elimu namna ya kuepukana nalo.
wa mkoa pia aliwataka viongozi wa dini kushirkiana na wadau katika kutoa elimu
kwa jamii kwani tatizo hilo linaweza kuwa historia kama elimu sahihi inaweza
kupatikana kwa wakati.
upande wake Mwakilishi wa Naibu Waziri wa Ofisi ya Waziri Mkuu kazi Vijana na
Watu Wenye ulemavu Joyce Maongezi alisema kwamba jamii inapaswa kutambua mapema
watoto wenye matatizo ya kichwa kikubwa na mgongo wazi.
kwamba ofisi yao itaendelea kutoa vifaa kwa watu wenye ulemavu ikiwemo
kuielimisha jamii pamoja na kuzindua mfuko wa Taifa wa watu wenye ulemavu ambao
utaweza kuwasaidia.
Halmashauri zitekeleze agizo la Serikali za kutaka watenge asimilia 2 ya mapato
yake kwa ajili ya watu wenye ulemavu “Alisema