Watanzania tunasumbuliwa na umasikini wa kifikra-dc hanang

Mkuu
wa Wilaya ya Hanang Mhe. Joseph Mkirikiti akizungumza na wananchi wa
kijij cha Gehandu wakati wa hitimisho la Maadhimisho ya Siku ya Mwanamke
anayeishi Kijijini yaliyofanyika kijiji hapo.


Wananchi
wa kijiji cha Gehandu wakimsikiliza Mkuu wa Wilaya ya Hanang Mhe.
Joseph Mkirikiti wakati wa hitimisho la Maadhimisho ya Siku ya Mwanamke
anayeishi Kijijini yaliyofanyika kijiji hapo.
Afisa
Maendeleo ya Jamii kutoka Wizara ya Afya- Idara Kuu ya MAendeelo ya
Jamii (kulia) akicheza ngoma ya Kibarabaigi na wanakijiji wa Kijiji cha
wakati wa hitimisho la Maadhimisho ya Siku ya Mwanamke anayeishi
Kijijini yaliyofanyika kijiji hapo.
Picha zite na Kitengo cha Mawasiliano WAMJW

………………


Na Mwandishi Wetu Hanang Manyara
Tanzania iliungana na nchi nyingine duniani kuadhimisha siku ya
kimataifa ya kuondoa umasikini duniani huku ikisemekana kuwa watanzania
walio wengi wanakabiliwa na umasikini wa kifikra zaidi kwa kukosa
kutambua firsa za kimaendeleo unaosababisha kuleta umasikini wa kipato.
 
Hayo yamebainika wakati wa hitimisho la Maadhimisho ya siku tatu
mfululizo ikiwa ni Siku ya Mwanamke anayeishi kijijini,Siku ya Chakula
Duniani na Siku ya kuondoa Umasikini Dunaini yaliyofanyika katika Kijiji
cha Gehandu Wilaya ya Hanang mkoa wa Manyara yaliyoratibwa na Wizara ya
Afya, Idara Kuu ya MAendeleo ya Jamii.
 
Akizungumza wakati wa hitimisho ya maadhiisho hayo Mkuu waWilaya
ya Hanang Mhe. Joseph Mkirikiti  amesema kuwa watanzania waliowengi
wanasumbuliwa na umasikini wa kifikra zaidi unaopelekea umasikini wa
kipato.
 
“Nitolee mfano katika Wilaya ya Hanang utakuta katika jamii sio
watu wanakosa pesa ila ni kukosa kutambua fikra za kuweza kujiwezesha
kiuchumi na kuondokana na  umasikini wa kipato” alisisitiza Mhe.
Mkirikiti
 
Ameongeza kuwa jambo kubwa linaloanisha umasikini ni ukosefu wa
fursa za kimaendeleo kwa jamii nyingi za kitanzania hivyo elimu
inahitajika kwa wananchi hasa wa vijijini hasa katika kutambua fursa za
kimaendeleo na kuzifanyia kazi.
 
Mhe. Mkirikiti amesema kuwa kwa upande wa Wilaya ya Hanang
umasikini wa kipato haupo ili kuna hitajika elimu wananchi ya jinsi ya
kutumia fursa za kimaendeleo kwa kutumia kipato wanachopata kujileta
maendeleo kwa kujenga nyumba bora na kupeleka watoto shule.
 
Akizungumza kwa niaba ya Wizara ya Afya- Idara Kuu ya Maendeleo
ya Jamii Mratibu wa maadhimisho kutoka Wizara hiyo Bi.Silyvia Siriwa
amesema kuwa mwanamke akiwezeshwa kiuchumi na kuondokana na umasikini
ana uwezo wa kulea familia na kupunguza masuala ya ukatili wa kijinsia
na unyanyasaji.
 
“Sisemi kama wanaume hawalei familia ila mwanamke akiwa na uwezo
wa kiuchumi kwa kiasi kikubwa anaweza kuiangalia familia kwa ukaribu
hasa katika malezi ya watoto” alisema Bi. Silyvia.