Rais magufuli awaonya wakimbizi wanaojihusisha na ujambazi

Rais
wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dk. John Pombe Magufuli amewataka
wakimbizi kutoka nchini Burundi ambao wamekuwa wakijihusisha na vitendo
vya kigaidi hapa nchini kuacha mara moja.



Rais
Magufuli ametoa onyo hilo alipokuwa akizungumza na wananchi wa maeneo
mbalimbali ya Mkoa wa Katavi baada ya kuweka jiwe la msingi katika
barabara ya Mpanda hadi Tabora na kuzindua kituo kipya cha mabasi
kilichopewa jina la Waziri Mkuu msataafu, Mizengo Pinda.

“Katika
mkoa huu kuna wenzetu kutoka Burundi na maeneo mbalimbali ambao
tuliwakaribisha katika nchi yetu kama Tanzania ilivyo na ukarimu kwa
watu kutoka nje lakini pamejitokeza baadhi ya changamoto watu wako
kambini baadhi yao wakawa wanashiriki katika masuala ya ujambazi
kulifanya eneo hili lisiwe salama kwasababu ya ukarimu wetu,

“Hauwezi
ukakaribishwa kwasababu ya shida ulizozitengeneza huko kwenu uje
uzilete hapa hivyo nitoe wito kwa ndugu zetu ambao walikuja hapa
tukawapokea kwa upole wasije wakalifanya eneo hili likawa la hatari,

“Hamuwezi
mkakaribishwa halafu baadhi yenu wanashiriki kuwaonea raia wema na saa
nyingine kupitisha silaha kupitia Ziwa Tanganyika ninawaomba waache na
kutokana na mienendo hiyo ambayo haifurahishi tumeona tulichunguze hili
suala la kuwapatia uraia watoto wao kwasababu wanaweza wakaleta watu
wakasema ni watoto wao kumbe ni majambazi kwani wamekuwa na tabia ya
kukaribisha wenzao wiki hii yuko hapa wiki inyokuja yuko Burundi na
kadhalika,

Aidha
amewataka Watanzania kuacha kuishi na raia hao wa kigeni kwa misingi
kwamba wanawasaidia katika kazi kwasababu wao wanakuwa wanawasoma halafu
usiku wanakuja, Tanzania ni nchi ya amani na palipo na amani kunakuwa
na kila kitu,” amesema Rais Magufuli.