Mwenyekiti wa uwt mhe. mary chatanda azindua mashindano ya dr. samia cup shinyanga, akabidhi vifaa vya michezo mshindi wa kwanza milioni 5

Na Mapuli Misalaba, Shinyanga

Mwenyekiti wa umoja wa wanawake wa chama
cha mapinduzi UWT Taifa Mhe. Mary Pius Chatanda amezindua ligi maalum ya DR.
SAMIA CUP SHINYANGA kwa ajili ya mashindano ya Mchezo wa mpira wa miguu katika
Wilaya ya Shinyanga mjini.

Uzinduzi huo umefanyika Jumamosi Agosti
26,2023 katika uwanja wa zimamoto (fire) Nguzonane mjini Shinyanga na
kuhudhuriwa na viongozi mbalimbali wa chama cha mapinduzi CCM wakiwemo wapunge
pamoja na madiwani katika Manispaa ya Shinyanga.

Akizungumza kwenye hafla hiyo Mwenyekiti
wa UWT Taifa Mhe. Mary Chatanda ameipongeza taasisi ya Bega kwa Bega kwa
ubunifu huo, kushirikiana na jumuiya ya umoja wa vijana wa chama cha mapinduzi
Wilaya ya Shinyanga mjini katika kuandaa mashindano ya mpira ambayo yatatoa
fursa za ajira kwa vijana watakao shirikia ligi hiyo.

Mhe. Mary Chatanda akiwa kwenye hafla ya
kuzindua ligi ya DR. SAMIA CUP SHINYANGA amekabidhi vifaa vya michezo ikiwemo
mipira pamoja na jezi zitakazotumiwa na timu 32 ambazo zinashiriki mchuano huo
ambao utafanyika kwa zaidi ya Mwezi mmoja.

Mwenyekiti wa Taasisi ya Bega kwa Bega
Mhe. Zainabu Shomar  amesema mashindano
hayo ni sehemu ya kuunga mkono juhudi za Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan katika
kuimarisha suala la michezo.

Mhe. Zainabu Shomar ambaye pia ni makamu
Mwenyekiti UWT Taifa amesema kuwa  baada
ya mchuano huo mshindi wa kwanza atachukua kombe na fedha Shilingi Milioni tano,
mshindi wa pili atachukua Shilingi Milioni tatu, na mshindi wa tatu atachukua
zawadi ya Shilingi Milioni mbili.

“Tumeandaa
mashindano hayo lengo ni kuunga mkono jitihada za Rais wetu Dkt. Samia Suluhu
Hassani na tunatarajia kukabidhi kombe na Milioni tano kwa mshindi wa kwanza
lakini mshindi wa pili tutampa Milioni tatu na mshindi wa tatu tutampa Milioni
mpili”.

“Kwa
sasa maadalizi yamekamilika kwa asilimia mia moja, vifaa vipo kila timu itakuwa
na jezi zake pamoja na mipira yake tumaamini hakuna changamoto itakayojitokeza”.
amesema
Mwenyekiti wa Bega kwa Bega Zainabu Shomar

Kwa upande wake Mbunge
wa jimbo la Shinyanga Mjini naibu waziri ofisi ya waziri Mkuu kazi,vijana,ajira
na wenye ulemavu Mhe. Paschal Patrobas Katambi
ametoa fedha Shilingi Milioni tano na Mipira 20 yenye
thamani ya Sh.milioni 1.6 kwa ajili ya kuunga mkono 
Mashindano
maalumu ya  DR. SAMIA CUP SHINYANGA.

Naye Mbunge wa
viti maalum Mkoa wa Shinyanga Mhe. Lucy Thomas Mayenga ametoa Shilingi Milioni
tatu kwa ajili ya kuunga mkono mashindano hayo ya DR. SAMIA CUP SHINYANGA
ambayo yameandaliwa na UVCCM kwa kushirikiana na Taasisi ya Bega kwa Bega.

 Mratibu wa mashindano ya DKT. SAMIA CUP SHINYANGA,  Jackline Isaro amemshukuru Mwenyekiti wa
umoja wa wanawake wa chama cha mapinduzi UWT Taifa Mhe. Mary Pius Chatanda kwa
kuzindua mashindano hayo.

Amesema mashindano DR. SAMIA CUP SHINYANGA
 yatatoa fursa mbalimbali kwa vijana na
kwamba  timu mbalimbali zikiwemo timu za
taasisi za serikali na taasisi binafsi katika Wilaya ya Shinyanga  mjini ikiwemo 
timu ya SHUWASA, timu za Bodaboda, timu za Masoko pamoja na timu za
Walimu.

Timu zilizopokea vifaa vya michezo kwa
niamba ya timu zingine, ni timu ya mpira ya chuo cha St. Joseph, timu ya
Ngokolo sekondari pamoja na timu ya Walimu.

Viwanja 8 vitakavyotumika katika
mashindano hayo ni uwanja wa Saba saba Kambarage mjini Shinyanga, uwanja wa
chuo cha ualimu Shinyanga (SHYCOM), uwanja wa kata ya Old Shinyanga, uwanja wa
shule ya msingi Kitangili, uwanja wa kata ya Ibadakuli, uwanja wa Jasko kata ya
Ngokolo, uwanja wa Ndala shule ya msingi pamoja na uwanja wa Joshoni kata ya
Lubaga katika Manispaa ya Shinyanga.

Mwenyekiti wa jumuiya ya
umoja wa vijana wa chama cha mapinduzi UVCCM Wilaya ya Shinyanga mjini Bwana
Jonathan Madete amewaomba wakazi wa Wilaya ya Shinyanga mjini kujitokeza kwa
wingi kwenye mashindano hayo ambapo  
kauli
mbiu inasema SAMIA VIWANJANI.

Mwenyekiti wa umoja wa wanawake wa chama
cha mapinduzi UWT Taifa Mhe. Mary Pius Chatanda akiwa katika zoezi la kuzindua
ligi maalum ya DR. SAMIA CUP SHINYANGA iliyoandaliwa na taasisi ya Bega kwa
Bega kwa kushirikiana na jumuiya ya umoja wa vijana wa chama cha mapinduzi
Wilaya ya Shinyanga mjini.

Hafla ya kukabidhi vifaa vya michezo
vitakavyotumiwa na timu 32 ikiendelea katika uwanja wa Zimamoto mjini
Shinyanga.

Viongozi, wadau mbalimbali na wananchi wa
Wilaya ya Shinyanga mjini wakiwa katika hafla ya kukabidhi vifaa vya michezo
vitakavyotumiwa na timu 32 kwenye mashindano ya DR. SAMIA CUP SHINYANGA ambayo
imeandaliwa na taasisi ya Bega kwa Bega kwa kushirikiana na jumuiya ya umoja wa
vijana wa chama cha mapinduzi UVCCM Wilaya ya Shinyanga mjini.