Na Said Mwishehe, Michuzi TV 

 WADAU wa sekta ya ubunifu katika fedha wakiwemo wakurugenzi wa kampuni changa ,watunga sera pamoja na wafanyabiashara wamekutana kupitia Fintech Happy Hour kwa lengo la kubadilishana uzoefu kuhusu ubunifu katika sekta ya fedha na kutafuta ufumbuzi wa changamoto zilizopo. 
Akizungumza wakati majadiliano hayo yaliyofanyika jijini Dar es Salaam Mwakilishi kutoka Shirika la Umoja wa Mataifa la UN CDF Aneth Kasebele ambaye ni Mtaalam wa Sera amesema wadau hao wametoka maeneo mbalimbali ya sekta ya fedha. 
“Pia leo tuko hapa na wawakilishi wa kampuni changa wanaoitwa Fintech, wawakilishi wa benki, watunga sera, Wanaowaklisha mamlaka za usimamizi na tumekuja kwa ajili ya Fintech ili wadau kwa pamoja tuangalie changamoto zilizopo na namna ya kuzitatua .Pia kukutana huku kunatoa fursa kwa walioshiriki kuanisha wadau muhimu wanaoweza kufanya nao kazi pamoja.
 “Lengo letu zaidi ni kuangalia jinsi gani wanaweza kukuza sekta ya Fintech ambayo moja kwa moja ni ubunifu katika sekta ya fedha Tanzania. Ndio tumeanza lakini tunaona tumefanikiwa kwa kiwango kikubwa kwasababu tumeona baadhi ya wawakilishi wanaotoka kwenye kampuni changa wamekuja kutuonesha biadhaa zao ambazo tayari ziko sokoni.” 
Aidha amesema ujumbe wa UN CDF ni kwamba ubunifu kwa Tanzania umeanza na unakwenda kwa kasi sana , kwa hiyo wameowamba wananchi wanaojihusisha na bunifu washiriki kwenye matukio kama hayo kwani yana fursa nyingi zikiwemo za kukutana na wawekezaji pamoja wabunifu, hivyo ni rahisi kujengeana uwezo.
 Kwa upande wake Meneja Uhusiano wa Kampuni ya Simu ya Infinix Erick Mkomoye amesema wanafuraha kuwa sehemu ya tukio hilo liliwakutanisha wabunifu katika sekta ya fedha kwani wao wamekuwa wahamasishaji wa kubwa wa matumizi ya teknolojia kupitia simu za mkononi za kampuni yao. 
“Infinix tunafahamu ulimwengu ambavyo umekuwa wa teknolojia zaidi, hivyo tunawahimiza vijana kuingia na kujihusisha zaidi na teknolojia ambayo inakuwa kwa kasi.Matukio ya aina hii kwetu ni muhimu kwasababu tunapata nafasi ya kuwasikiliza wadau kuhusu nini kifanyike kwenye kukuza utumiaji wa teknolojia nchini,”amesema. 
Ameongeza wanafahamu kuna maeneo mbalimbali yanayohitaji ukuaji wa teknolojia kama kwenye afya, kilimo pamoja na biashara.Hivyo wanawasilikiza na kuangalia ni kwa namna gani wataboresha huduma na kwa jicho la kipekee kuzikuza ili kufukia malengo.
“Tutaendelea kushiriki kwenye matukio ya aina hii na ujumbe wao mkubwa siku zote unasema Wakati ni sasa na ndio wakati wa vijana kuamka kuhakikisha wanatumia teknolojia katika biashara zao.” 
Wakati huo huo Mkurugenzi wa Kilimo Maendeleo Mathew Ngwahi amesema kilimo maendeleo ni jukwaa ambalo limeanzishwa na vijana wa kitanzania na limejikita katika kuangalia wakulima wanatambulika na wanafikiwa na huduma mbalimbali ikiwemo huduma za pembejeo na mikopo na bima kupitia mifumo ya kidigitali.
 “Tuko hapa kwa ajili ya kuelezea huduma ambayo tunaitoa kwa wakulima , kwa sasa hivi tunafanya kazi kwenye wilaya 16 nchini na tumewafikia wakulima 83000.Tumewafikiwa wakulima hao kutokana na msaada mkubwa tunaupata kupitia program ya UN CDF hasa katika kuhakikisha tunatengeneza bidhaa ambazo ni bora kabisa kwa ajili ya wakulima na kuwahudumia kwa viwango ambavyo vinatakiwa.” 
Aidha amesema Kilimo Maendeleo wanatamani kuona jamii inatambua kuwa dunia inabadilika na teknolojia inatumika sasa hivi katika maisha ya kila siku, kwa hiyo hawategemei kuona watu wanaendeelea kushika fedha mkononi, fedha inakaa kwenye simu , zinakaa kwenye waleti za fedha kidigital, kwa hiyo kuna mambo mengi yanaendelea kwenye mtandao. 
Kwa upande wake Franc Israel ambaye ni Mmoja ya Waanzilishi wa Kampuni ya kampuni ya Afya Lead ambayo ni miongoni mwa kampuni changa amesema wamekuja na ubunifu kwenye sekta ya afya na kwa sasa wanabunifu zao tatu ikiwemo Pamoja Bima inayorahisisha malipo ya bima ya afya ya jamii kupitia simu za mkononi.
 “Hii bidhaa ilianza kwa kuangalia idadi kubwa ya Watanzania hawatumii bima ya afya lakini tunaona juhudi za Serikali za kuhakikisha bima ya afya inakuwa kwa watu wote.Hivyo tumekuja na hii bidhaa ili kurahisha malipo ya bima kwa kutumia simu ya mkononi,”amesema.
 Aidha Mkurugenzi wa Kampuni ya Settlo Teknologies Mohamed Awami amesema wamekuwa wakisaidia wafanyabiashara wadogo kukua kwa wepesi na wamekuwa wakitumia ulimwengu wa kidigitali kutoa huduma kwa kutumia simu ya mkononi ambako kuna App maalumu ya Settlo Teknologies. 
 “Tunao wafanyabiashara zaidi ya 2000 ambao wamejiunganisha na huduma zetu kupitia App ya Settlo Teknologies. Tunajivunia namna ambavyo wafanyabiashara wamejiunga na huduma zao wanaona mafanikio makubwa.Ombi letu kwa wadau wote tunayo sababu ya kuunganisha nguvu katika kuwasaidia wafanyabiashara wa kada mbalimbali hasa wajasiriamali .  Hatuko kwasababu ya kushindana bali tuko kwa ajili ya kuunganisha nguvu na kusaidiana.” amesema.
 Mwakilishi kutoka Shirika la Umoja wa Mataifa la UN CDF Aneth Kasebele ambaye ni Mtaalam wa Sera akifafanua jambo kwa wadau wa sekta ya ubunifu katika fedha.

Mwanzilishi wa Kampuni ya Afya Lead ambayo imekuja na ubunifu katika sekta ya afya Franc Israel akielezea huduma wanazotoa katika kuhakikisha watanzania wanafanya malipo ya biama ya afya ya jamii kwa kutumia simu za mkononi.
04:Baadhi ya wadau wakifuatilia majadiliano wakati wa Fintech Happy Hour iliyoandaliwa na Shirika la Umoja wa Mataifa la UN CDF
Mwakilishi kutoka Shirika la Umoja wa Mataifa la UN CDF Aneth Kasebele ambaye ni Mtaalam wa Sera(kulia) akijadliana jambo wakati wa majadiliano yaliyowakudanisha wadau mbalimbali wakiwemo wabunifu katika sekta ya fedha.
Mwanzilishi wa Kampuni ya Afya Lead ambayo imekuja na ubunifu katika sekta ya afya Franc Israel akielezea huduma wanazotoa katika kuhakikisha watanzania wanafanya malipo ya biama ya afya ya jamii kwa kutumia simu za mkononi.
Mkurugenzi wa Kilimo Maendeleo Mathew Ngwahi akizungumza wakati wadau mbalimbali wa sekta ya fedha na ubunifu walipokutana jijini Dar es Salaam kwenye Fintech Happy Hour ambapo ametumia nafasi hiyo kuelezea hatua kwa hatua namna ambavyo jukwaa la Kilimo Maendeleo linavyowasaidia wakulima katika wilaya 16 nchini

 .

 

05: Mwakilishi kutoka Shirika la Umoja wa Mataifa la UN CDF Aneth Kasebele ambaye ni Mtaalam wa Sera akifafanua jambo kwa wadau wa sekta ya ubunifu katika fedha.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *