Na mwandishi maalum
Naibu Katibu mkuu huduma za jamiiWanawake na WatotoKanisa la KKKT Tanzania Mch Rachel Axhweso amesema moja ya vikwazo vikubwa vinavyochangia mimba za ujana ni kutokuwepo Kwa waajiriwa wataalamu wa ushauri nasaha katika maeneo ya shule .
Mimba za ujana kama kadhia kubwa inayowakumba baadhi ya vijana Katika umri mdogo baadhi ya wadau wamekuwa wakieleza kuwa ni mimba zisizo tarajiwa.
Katika mahojiano maalumu na Mchungaji Axhwesso alieleza kuwa vijana wengi, hususan wa kike, hupata changamoto za mimba za mapema zinazowapoteza katika malengo yao ya maisha kutokana na kuanza kulea watoto wakati wao wakiwa bado watoto .
Pia alieleza kuwa suala la uangalizi wa watoto wa kike limekuwa changamoto kwa sasa vijana wa kike wamesusiwa na makanisa hayawajalia kwa kuwapa mafundisho, shule haziwajibiki ipasavyo kwa kuwafuatilia na hata wazazi wamesahau wajibu wao .
Kwa mujibu wa ripoti ya utafiti wa afya ya uzazi na mtoto na viashiria vya Malaria, uliofanyika mwaka 2015-2016 na Ofisi ya Takwimu ya Taifa, Ofisi ya Mtakwimu Mkuu wa serikali, Wizara ya Afya Maendeleo ya Jamii Tanzania na Wizara ya Afya ya Zanzibar, unaonesha kuwa asilimia 27 ya wanawake walio katika hatua ya ujana, tayari wana watoto nawengine ni wajawazito.(TDHS-MIS 2015-2016)
Ripoti hiyo, pia imebainisha kuwa wanawake vijana wasio na elimu wana uwezekano wa kuzaa mapema mara tano zaidi ya wale walio na elimu ya sekondari au zaidi na kutaja kuwa uzazi wa umri mdogo unatofautiana kwa kuzingatia utajiri wa kaya kwa asilimia 13 na asilimia 42 kwa wale walio katika kaya maskini
Moja ya fatiti zinaonesha kuwa Jumla ya asilimia 52% ya wasichana wasio na elimu wametajwa kupata mimba za ujana ikiwa ni Katika hatua ya ukuaji,ambapo kila mtu hupitia .kutokana na Hali hiyo vijana wamejikuta wakiwa Katika majukumu kabla ya kuanza kupanga na kumudu majukumu ya utu uzima, yakiwemo ya kuwa na familia.
ni vipi vikwazo vinavyokwamisha kumaliza kadhia ya Mimba za ujana Mch Rachel Axhweso anatoa ufafanuzi na kueleza athari pia ni Nini kifanyike
……sauti .Mch Rachel Axhweso…….
Jamii haina budi kukitazama Kundi la Watoto wa kike kwa ukaribu zaidi Ili kuhakikisha kuwa wanadhibiti mimba za ujana na kuandaa Taifa lenye Nguvu na maarifa.