Amshambulia mpenzi wake wa zamani baada ya kumnasa akipanga mipango ya kuolewa na bwana mwingineMkulima wa Kijiji cha Nangaru, mkoani wa Lindi Abdallah Shaibu Nyuki (30), amehukumiwa na Mahakama kuu ya Tanzania Kanda ya Mtwara, kwenda jela miaka 8, baada ya kupatikana na makosa 2 ya kutaka kuuwa bila kukusudia.


Akitoa hukumu hiyo Jaji Mfawidhi Mkuu wa Mahakama hiyo Joel Paul Ngwembe, amesema anamhukumu mshtakiwa kifungo cha miaka 4 kwa kosa la kwanza la kujaribu kuua na miaka 4 tena kwa kosa la kujeruhi.


Awali Mwanasheria wa Serikali, Emmanuel John amesema kuwa mshtakiwa akiwa na panga mkononi Disemba 08, 2018, aliwashambulia Hashimu Bakari Mnocho na Zakia Salum Kindumba, ambaye ni mwanamke aliyeachana naye, baada ya kuwakuta wako pamoja wakizungumzia mipango ya ndoa.


Mwanasheria huyo amesema kuwa baada ya kuwakuta wakiwa wanazungumza mshtakiwa akiwa na panga mkononi aliwajeruhi kwa kuwashambulia mwilini, ambapo baada ya kufanya tukio hilo alikimbia Kijiji cha jirani.
Chanzo- EATV