Mkuu wa wilaya ya Monduli mhe.Edward Jonathan Balele akizungumza na wageni waalikwa katika Uzinduzi wa Taasisi isiyo ya Kiserikali ya Vuka Initiative iliyofanyika katika hotel ya Corrido spring Jijini Arusha.
Mkurugenzi a mwanzilishi wa Taasisi ya Vuka Initiative Bi Veronica Ignatus Boniface akisoma risala mbele ya mgeni rasmi katika siku ya Uzinduzi wa Taasisi hiyo 18)9/2020 iliyofanyika katika hotel ya Corrido Spring mkoani Arusha
Bi Kabula Sukwa katibu mtendaji wa Taasisi ya Vuka Initiative akiteta Jambo na wageni waalikwa siku ya Uzinduzi wa Taasisi hiyo uliofanyika mkoani Arusha.tar 18/9/2020
Afisa Maendeleo Mkoa wa Arusha bi.Blandina Nkini akizungumza katika Uzinduzi huo
Mkurugenzi wa Taasisi ya Vuka Initiative Bi Veronica Ignatus akimkabidhi mgeni Ambaye Ni Mkuu wa wilaya ya Monduli Mhe.Edward Jonathan Balele risala,kulia kwake ni Katibu mkuu Vuka Initiative Kabula Sukwa pamoja na Afisa Maendeleo mkoa wa Arusha Bi Blandina Nkini
Mkuu wa wilaya ya Monduli mhe.Edward Jonathan Balele kwa kushirikiana na baadhi ya viongozi wa Vuka Initiative wakikata keki kwa pamoja ishara ya kuzinduliwa rasmi kwa Shirika Hilo pamoja na Kampeni ya “Mwogeshe mwanao
Wa kwanza kulia Ni Mkurugenzi wa SASA Foundation bi Jovita kulia kwkae ni Wakili Mary Mwita katika hafla ya Uzinduzi wa Taasisi ya Vuka Initiative
Baadhi ya wagenj walioalikwa katika Uzinduzi wa Taaasis ya Vuka Initiative uliofanyika Jijini Arusha
Wageni waalikwa katika uzinduzi huo wakifuatilia kwa makini kile kinachoendelea
Wageni waalikwa katika uzinduzi huo wakifuatilia kwa makini kile anachozungumza mkuu wa wilaya ya Monduli .
Shughuli ya uzinduzi ikiendelea ,wageni waalikwa wakiendelea kufuatilia
Mkuu wa wilaya ya monduli Edward Jonathan Balele akipokea kipande cha keki kutoka kwa mkurugenzi wa Taasisi ya Vuka Initiative bi Veronica Ignatus mara baada ya zoezi la uzinduzi rasmi kukamilika
Shamrashamra zikiendelea baada ya mkuu wa wilaya ya Monduli kuzindua rasmi Taasisi ya Vuka Initiative
Mkurugenzi wa Vuka Initiative bi Veronica Ignatus akipongezana na Katibu wa Taasisi hiyo bi Kabula Sukwa mara baada ya uzunduzi rasmi uliofanyika jijini Arusha mwishoni mwa wiki
Na Mwandishi wetu,Arusha.
Wazazi /Walezi wametakiwa kutenga muda ,kujenga ,Upendo,ukaribu kwa watoto wao ili kutambua mabadiliko yanayojitokeza, kuwasikiliza na kubaini changamoto wanazozipitia pamoja na mienendo yao ili waweze kuwasaidia kabla ya tatizo kuwa kubwa
Amesema hayo Mkuu wa wilaya ya Monduli Mhe.Edward Jonathan Balele aliyemuwakilisha Mkuu wa mkoa wa Arusha mhe.Iddy Kimanta katika Uzinduzi wa Taasisi isiyo ya Kiserikali ya Vuka Initiative uliofanyika tar 18/9/2020 katika Hotel ya Corrido Spring na kuhudhuriwa na Viongozi mbalimbali wa Taasisi za serikali na zisizo za Kiserikali
Mhe. Balele alisema kuwa kazi ya kuitumikia jamii ni ngumu na inahitaji msaada wa Mungu,hivyo Taasisi hiyo imechagua fungu jema katika kuungana na Serikali kuhamasisha mapambano dhidi ya vitendo vya Ukatili wa Kijinsia kwa wanawake ,wasichana,
watoto na jamii kwa ujumla.
Aidha ameipongeza Taasisi hiyo ya Vuka Initiative kuja na Kampeni ya ”Mwogeshe Mwanao”ambapo alisema kwamba imekuja kwa wakati sahihi kwani jamii umejisahau katika malezi ya watoto ambapo muda mwingi wamekuwa wakiutumia katika utafutaji na kusahau majukumu ya kifamilia.
“Kampeni hii imenikumbusha mwaka 1997wakati mke wangu amejifungua mtoto wetu wa kwanza ,alijifungua kwa kufanyiwa upasuaji,hatukuwa na msaidizi hivyo ilibidi nijifunze,majukumu yote yalikuwa kwangu,kumuangalia mama,kumuhudumia mtoto wetu pamoja na Mambo mengine pia inatukumbusha wajibu wetu Kama Walezi na wazazi kwa ujumla wetu.”alisema Balele.
Alisema kuwa Kampeni hiyo imemgusa kwani katika wilaya ya Monduli kumekuwa na tatizo kubwa haswa jamii ya wafugaji kwa kuwatesa wake zao, ila jamii ikishirikiana kwa pamoja italeta maendeleo na itaepusha migogoro inayoibuka kila mara na kusababisha kudumaa kwa uchumi katika familia na jamii kwa ujumla.
” Balele:Siku moja nilipita Makuyuni,mama mmoja alinishika bega
akilia akaniambia,mimi niliolewa nikiwa na umri wa miaka 12, na alikaa kwa mumewe miaka 5, wakafanikiwa kupata mtoto wa kwanza,akabeba ujauzito wa pili ukiwa na miezi 6 ,mumewe alimpiga kwa fimbo tumboni akapata maumivu makali mnokisha akamfukuza bila kuwa na msaada, akakimbilia msituni Engaruka , akajifungua mtoto akiwa amefariki,bila kupata msaada na wa mtu yeyote,alikaa porini kwa zaidi ya mwezi mmoja, ikampelekea kiakili kuonekana kuathirika hata kuonana na watu akawa anaogopa mno
…Lakini ilitokea kijana mmoja mfugaji kila siku akipita watu walikuwa wakisema kuwa yule mama ni kichaa kumbe sivyo!akachukua nafasi ya kumfuatiliana na kwenda kukaa nae nyumbani kwao akaanza kurudi katika hali yake ya kawaida kwa miaka 10 kati ya miaka 8 aliyoachwa na mumewe yule wa kwanza,akapata ujauzito tena akajifungua mtoto wa kike ambapo mtoto sasa ana miaka 2 na miezi 3,cha kushangaza zaidi yule baba aliyemuacha miaka 10 iliyopita safari hii anakuja kumchukua mtoto na yule mtoto alipewa na akaondoka nae.
Mhe.Balele anasema kuwa baada ya yeye kupata taarifa hiyo aliamua kuacha kila kitu na akafunga safari kuelekea Engaruka ,na kufikia mji anapokaa mama yule na hatua nyingine za kisheria zilifuata ikiwa ni pamoja na kuhakikisha kuwa yule mama anapata nyumba ya kuishi pamoja na changamoto zote alizopitia, lazima maisha yaendelee,anasema katika mila na desturi za jamii ya kimaasai alichokifanya huyo mwanaume inaonekana ni sahihi kabisa kwa mujibu wa mwanamke wa jamii hiyo.
Kwa upande wake Mkurugenzi na mwanzilishi wa Taasisi ya Vuka Initiative Bi.Veronica Ignatus alisema kuwa wanajishughukisha na utoaji wa Elimu itakayowajengea uwezo wanawake,wasichana na watoto pamoja na kuhamasisha mapambano dhidi ya Ukatili wa Kijinsia kwa wanawake na waatoto
Bi.Veronica alisema kuwa Taasisi hiyo ni changa bali wanayo malengo makubwa ya kuanza shughuli za kuitumikia jamii na kusaidia serikali ya awamu ya tano ya Rais John pombe Magufuli ya kuboresha Maisha ya Watanzania,kwani kumuelimisha mwanamke na watoto ni kuiwezesha jamii na Taifa kwa ujumla.
Akizungumza Kampeni ya “Mwogeshe Mwanao”iliyopo
ndani ya Taasisi hiyo Veronica alisema imelenga kupunguza changamoto za Ukatili na Unyanyasaji wa kijinsia katika jamii,Ikiwemo iutambua aina mbalimbali za ukatiliwa kijinsia kwa wanawake ,wasichana,watoto na jamii nzima.
Pia Kampeni hiyo inalenga kuwakumbusha wazazi/Walezi na jamii kwa ujumla kuhusu jukumu la kuongeza ukaribu,uoendona mahusiano kwa watotona kutenga muda wa malezi na ufuatiliaji wankaribu kwa watoto.
Bi.Veronica alisema kuwa chanzo kikubwa cha ukatili wa kijinsia ni pamoja na mila na desturi mbaya ,mfumo dume,uelewa mdogo kuhusu sheria na haki za binadamu,imani potofu,kutokuwajibika kwa viongozi ,elimu duni ,ushirikina na sera na sharia kandamizi.
Aidha alisema kuwa wanatarajia kufikia watoto,na wanawake katika makundi kama wafanyakaziwa Sekta rasmi na zisizo rasmi ,mathalani mama lishe, wajasiriyamali,wa
viwandani,wauza mahindi na n.k ambapo wamepanga kuanza na wilaya sita za mkoa wa Arusha Ikiwemo (W)Arusha mjini,Arumeru,Karatu,,Longido ,Ngorongoro na Arusha DC.
Bi.Veronica alisema kuwa msingi wao umekuja baada ya kugundua kuwa watoto wengi huathirika kwa kupigwa na kutendewa ukatili na unyanyasaji na watu wa karibu yao kama ndugu,jamaa,marafiki wenzao na hata shuleni
Aidha amesema kuwa Taasisi hiyo inaungana na mpango wa Taifa wa kutokomeza ukatili dhidhi ya wanawake na watoto kwa lengo la kupunguza kwa kiwango cha 50% ifikapo 2022 ambapo mpango huo ni sehemu ya utekelezaji wa sera ya maendeleo ya wanawake na jinsia ya mwaka 2000,mkakati wa Taifa wa maendeleo ya jinsia ya mwaka 2005,sera ya maendeo ya watoto ya mwaka 2008,sheria ya makosa ya kujaamiana ya mwaka 1998
Taasisi ya Vuka Initiative imesajiliwa kisheria kwa no 00NGO/R/1149 Kama Shirika lisilo la Kiserikali chini ya Sheria ya Mashirika yasiyo ya Kiserikali namba 24 ya mwaka 2020 kifungu namba 12(2).