Mwenge wa uhuru wakataa mradi wa maji njombeNa Amiri Kilagalila-Njombe


Mbio
za mwenge wa uhuru kitaifa mwaka 2019 zimeshindwa kuweka jiwe la msingi
katika ujenzi wa mradi wa maji kijiji cha Kidegembye jimbo la Lupembe
wilayani Njombe mkoani Njombe.
Akizungumza
na wananchi mara baada ya kukagua na kupitia nyaraka za ujenzi wa mradi
huo amesema mwenge wa uhuru umeshindwa kuweka jiwe la msingi katika
mradi huo kutokana na kubaini ukiukwaji wa utaratibu wa ujenzi.
“Baada
ya kufanya uchaguzi wa kina,tumeona chest ya nondo milimita nane
haijapimwa lakini pia zege ya kati kati haijapimwa,sambamba na hilo
kwenye pampu house zege imetumika na haijapimwa kwa hiyo maana yake hapa
utaratibu wa kiujenzi umekiukwa,hivyo basi mbio za mwenge wa uhuru
kitaifa hazitoweza kuweka jiwe la msingi katika mradi huu”alisema Mzee
Mkongea
Aidha
amesema licha ya kuwa Mwenge wa uhuru umeshindwa kuweka jiwe la msingi
katika mradi huo,bado maji katika mradi yapo safi na salama na kuomba
wananchi kuyatumia.
“Lakini
maji yapo safi na salama ndugu wananchi muweze kuyatumia hayana shida
yoyote,hitilifa ambayo imejitokeza hapa ni kwa wataalamu kuto kuweza
kusimamia vizuri kwasababu hizi ni fedha za wananchi lazima zisimamiwe
kipengele hadi kipengele”aliongeza kiongozi wa mbio za mwenge
Katika
hatua nyingine kiongozi huyo wa mbio za mwenge amemuagiza mkuu wa
wilaya ya Njombe Ruth msafiri kumkabidhi taarifa ya mradi huo afisa
takukuru na kuichunguza kwa umakini na kuipeleka nakala hiyo baada ya
wiki mbili makao makuu ya takukuru.
Awali
akisoma taarifa ya mradi huo Injinia wa maji halmashauri ya wilaya ya
Njombe Rajabu Yahaya kwa niaba ya mkurugenzi,amesema hali halisi ya
utekelezaji wa mradi huo umefikia asilimia 90% ya kukamilika ambapo
mpaka sasa wananchi wanapata huduma ya maji huku mradi huo ukiwa umeanza
kutekelezwa machi 7,2018 na mkandarasi MSSTC construction limited kwa
gharama ya shilingi bilioni moja mia tatu hamsini na nne elfu, mia tatu
na nane mia nane sitini na nne pamoja na thamani.
Takribani
miradi sita imekaguliwa na kufunguliwa na mbio za mwenge wa uhuru
kitaifa wilayani Njombe mkoani Njombe huku kiongozi wa mbio za mwenge
akitoa pongezi kwa halmashauri hiyo katika utekelezaji wa miradi.