la Iran (IRGC) limerusha makombora ya balestiki na kupiga kambi za
kijeshi za Marekani nchini Iraq, kama jibu la kuuawa Jenerali Qassem
Soleimani, aliyekuwa Kamanda wa Kikosi cha Quds cha SEPAH.
Taarifa ya IRGC imesema kuwa, Iran imetoa jibu hilo kwa Marekani
alfajiri ya leo, ambapo imelenga uwanja wa ndege wa kijeshi wa Marekani
wa Ain al-Assad katika mkoa wa al-Anbar, magharibi mwa Iraq.
Jeshi la Iran limeitaka Marekani iwaondoe wanajeshi wake wote katika
nchi hiyo ya Kiarabu, likisisitiza kuwa halitatenganisha kati ya
Marekani na Israel katika kujibu mapigo ya kuuawa Jenerali wao.
Waziri wa Mambo ya Nje wa Iran, Mohammad javad Zarif amezungumzia
kuhusu jibu hilo la Iran katika ujumbe alioutuma kwenye ukurasa wake wa
Twitter na kuandika: “Iran imechukua hatua madhubuti ya kujihami kwa
mujibu wa Sura ya 51 ya Mkataba wa Umoja wa Mataifa kwa kulenga kambi ya
jeshi ambayo ilitumiwa katika shambulizi la kioga dhidi ya raia na
maafisa wetu wa ngazi za juu. Hatutaki kukuza mambo wala vita, lakini
tutajihami dhidi ya uvamizi wowote.”
Wizara ya Ulinzi ya Marekani (Pentagon) imethibitisha habari hizo za
kuvurumishwa makumi ya makombora ya balestiki kuelekea katika kambi ya
jeshi la Marekani nchini Iraq.