Waziri wa Madini Dkt Doto Biteko akisaini kitabu cha wageni alipotembelea banda la maonyesho la Kampuni ya Gf Truck Group kwenye maonyesho ya Madini yanayoendelea mkoani humo. |
Na David John Geita
WAZIRI wa Madini dkt.Doto Biteko ameyataka makampuni mengine nchini kuiga mfano wa Kampuni ya Gf Truck Group kwa kitendo chao cha kuunga juhudi za Serikali katika kuwaletea wananchi wake maendeleo.
Waziri Beteko ameyasema hayo leo Ocktoba 1, mwaka huu mkoani geita kwenye maonyesho ya tano ya kitaifa ya teknolojia ya uwekezaji wa madini yanayoendelea mkoani humo mara baada ya kutembelea kwenye banda la Gf Truck Gruop ambao walikuwa Gf Truck Gruop Day ambapo walitumia siku hiyo kuendesha zoezi kuchangiaji damu kwa kushirikiana na Damu salama.
Amesema kuwa Gf Truck Group wanapaswa kupongezwa kwa hatua yao ya kuendesha zoezi hilo kupitia maonyesho hayo ya tano ya teknolojia ya madini nakwamba moja ya jambo ambalo serikali wanalisukuma lifanyike nikuwafanya watanzania washiriki kwenye uchumi wa madini na katika hilo kuna watu wapo kwenye kilimo,Madini,na wengine kwenye mifugo hao wote waone uwepo wa madini ni fursa kwao ili kukuza uchumi wao.
Gf Truck tunawapongeza sana hususani kwa siku yenu ya leo umeonyesha jambo kubwa la kuchangia damu na tunawatakiwa kila la heri na hapa naomba nitowe wito kwa watanzania wengine tuchangie damu kwa ajili ya kuokoa maisha ya wezetu.”
Nakuongeza kuwa “Gf Truck wameonyesha mfano na nitowe kwa kampuni nyingine pamoja na kufanya maonyesho lakini kuna kitu ambacho kinagusa maisha ya watu moja kwa moja hivyo Mungu awabariki asanteni sana.”amesema Waziri Biteko
Kwaupade wake Meneja Mawasiliano wa Kampuni hiyo ya Gf Truck Smart Deus akizungumza mbele ya Waziri Biteko amesema kuwa wameendesha zoezi hilo ikiwa ni kuwarudishia jamii katika kile ambacho wanakipata.
Amesema kuwa anaamini yeye pamoja na kampuni yake jambo ambalo wamelifanya linakwenda kuacha alama kubwa hususani kwa wananchi wa mkoa wa geita.
Kwaupande wake Mshauri wa Damu salama kutoka Hospitali ya rufaa Mkoani humo Halima Juma amesema kuwa tangu kuaza kwa maonyesho hayo Septemba 27 mwaka huu hadi kufikia leo Oktaba mosi wamefanikiwa chupa 148 za damu.
Pia katika hatua nyingine Halima kupitia Gf Truck Group Day amesema kuwa watu ambao wamewafikia katika kuchangia Damu Salama ni pamoja na watu wa boda boda,na wasanii na wananchi waliohamasika kupitia Kampuni ya Gf Truck Group ni 75 na kati ya hao waliofanikiwa kuchangia damu ni 25 na 50 waliobaki hawakufanikiwa kutokana na sababu mbalimbali.
“Tunashukuru Gf Truck Group kwa mchango wao kwenye timu ya damu salama na hospitali kwa ujumla kwa kuchangia viburudisho,na tishert kwa wachangiaji wakimo watumishi wa Damu salama.