Katibu tawala wa mkoa wa Iringa Happines Seneda amepongeza jitihada zinazofanywa na chama kikuu cha ushirika wa wakulima cha mkoa wa Iringa -IFCU 1998(LTD kwa kuwakomboa wakulima kwa kuagiza mbolea kutoka nje.
Seneda amesema hayo jana katika kijiji cha Isalavsnu Mufindi wakati akizindua wa uuzaji wa mbolea ya mkulima iliyoagizwa na chama hicho mkoa wa Iringa .
Alisema kwa Tanzania ni mikoa miwili pekee ambayo imeweza kuwa na vyama bora za wakulima kwa kuwaagizia wakulima mbolea kutoka nje na kutaka mbolea hiyo kuwafikia wakulima.
Alisema hatua kubwa imepigwa ndani ya mkoa wa Iringa kwa kuwa na Nguvu kubwa na kuagiza vyama vyote kuungana ili kuwa pamoja na kunufaika na mpango huo .
Seneda alisema kuwa mbolea hiyo unapaswa kuuzwa kwa wakulima wadogo na marufuku kuuzwa kwa wakulima wa kati ama madalali kuingilia kati .