Iran yalaani mashambulizi ya marekani iraq na syria

Iran
imelaani mashambulizi ya anga yaliyofanywa na Marekani nchini Iraq na
Syria dhidi ya wanamgambo wa Kataib Hezbollah wanaoungwa mkono na Iran.

Msemaji
wa Wizara ya Mambo ya Nje ya Iraq, Abbas Mousavi amesema wanalaani
vikali uchokozi wa Marekani katika ardhi ya Iraq na vikosi vya Iraq na
wanauona kama mfano wa wazi wa ugaidi. 
Waziri
wa Ulinzi wa Marekani, Mark Esper alisema jana vikosi vyake vilifanya
mashambulizi yaliyowalenga wanamgambo wa Iraq wanaoungwa mkono na Iran,
wakiwalaumu kwa shambulizi la roketi lililomuua mkandarasi wa
Kimarekeni. 
Esper
amesema Marekani imeyashambulia maeneo  matatu ya magharibi mwa Iraq na
mawili mashariki mwa Syria, ikiwemo maghala ya silaha na kambi
zinazodhibitiwa na wanamgambo. 
Waziri
wa Mambo ya Nje wa Marekani, Mike Pompeo amesema mashambulizi hayo ni
ujumbe kwamba Marekani haitovumilia vitendo vyovyote vya Iran ambavyo
vinahatarisha maisha ya Wamarekani.