Israel yatoa onyo kama itashambuliwa na iran

Waziri
mkuu wa Israel Benjamin Netanyahu ameonya kwamba nchi yake italipiza
kisasi kwa yoyote atakayewashambulia, huku akirejelea matamshi yake ya
kuiunga mkono hatua ya Marekani ya kumuua mkuu wa kikosi maalumu cha
Iran Jenerali Qassemi Soleimani wiki iliyopita. 

Amesema
mjini Jerusalem kwamba yoyote atakayewashambulia atakabiliwa na hatua
kali ya kulipiza kisasi na kuongeza kuwa Israel inasimama kikamilifu na
uamuzi wa rais wa Marekani Donald Trump na kuongeza kuwa anahitaji
kupongezwa kwa kuchukua hatua hiyo kwa utaratibu, ujasiri na umadhubuti.