Jeshi la polisi laonya wahalifu kutothubutu kuingia mitaani sherehe za mwaka mpya

Na Ahmed Mahmoud Arusha

JESHI
la Polisi mkoa wa Arusha, limesema Arusha sio sehemu salama wala ya
kupumzikia kwa majambazi,wahalifu na Vibaka bali ni sehemu salama kwa
raia wema tu.



Pia 
Kamanda Jonathan Shana, ametuma salamu kwa Majambazi, wahalifu na
Vibaka, kwamba sumu haionjwi na wakitaka kujaribu basi watainywa halafu
watatambua uzuri wake.

Kamanda
Shanna, ameyasema hayo  leo  ikiwa ni maandalizi ya kuupokea waka mpya
2020 ambao utaanza rasmi saa 6.00 usiku na kuoengeza kwamba Jeshi la
polisi limejipanga kuimarisha ulinzi na usalama kwenye mkesha wa mwaka
mpya .

Amesema
Jeshi  la polisi litaendelea kufanya kazi ya kuhakikisha usalama na
amani ya kudumu inaendelea kuwepo mkoani Arusha wakati wowote  na
kuwataka wananchi kuendelea na shughuli zao kama kawaida.

Kamanda,Shanna,amesem
Jeshi hilo litaendelea kufanya kazi zake  bila kulala wala kupumzika na
limejipanga kuimrisha doria maeneo yote yenye mikusanyiko ya watu hasa
nyakati za usiku kwenye maadhimisho ya kuupokea mwaka mpya2020.

Kamanda
Shanna,amewahakikishia wananchi wote kwamba Arusha itakuwa shwari
kipindi chote cha siku kuu na baada ya siku kuu na akawaonya Vibaka na
wahalifu wengine kutafuta pa kwenda kwa kuwa Arusha hakuna nafasi hiyo.

Amelipongeza
jeshi la polisi kwa kuimarisha ulinzi na usalama kwa kudhibiti matukio
yote ya uhalifu,ujambazi na udokozi kwa kipindi chote cha mwaka mzima
kuanzia January hadi Desemba 31 mwaka 2019.

Amewaambia
kuwa kazi waliyoifanya tangia January mosi mwaka 2019 wanaihitimisha
Desemba 31 saa 6.00 usiku  na wataanza upya kazi ya ulinzi na usalama
kuanzia saa 6.01 usiku mwaka 2020