Jeshi la sudani lazima jaribio la mapinduzi

Jeshi
la Sudan linayashikilia makao makuu ya kikosi cha usalama wa taifa cha
nchi hiyo ambacho awali kilikuwa kitiifu kwa rais aliyepinduliwa Omar
al-Bashir, ripoti zinaeleza.


Mapambano
yalianza Jumanne katika jiji la Khartoum ambapo milio ya milipuko
ilisikika. Kitengo hicho cha usalama wa taifa kwa sasa kinavunjwa.

Serikali
inadai kuwa uasi huo umechochewa na malipo ya mafao, lakini pia kuna
mashaka juu ya tukio hilo kulenga kuchelewesha mabadiliko ya kisiasa
nchini humo.

Kiongozi
mwandamizi wa baraza huru linaloongoza Sudan kwa sasa, Jenerali
Mohammed Hamdan Dagalo, amemtuhumu mkuu wa zamani wa usalama wa taifa
Salah Gosh kuwa yupo nyuma ya uasi huo.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *