Mahakama ya Rufaa imeamua kuwa Mrakibu Mwandamizi wa Jeshi la Polisi (SSP) Christopher Bageni atanyongwa hadi kufa.
Uamuzi huo umetolewa leo, Dar es Salaam na ndiyo unahitimisha mwenendo wa kesi yake. Hii maana yake ni kwamba Bageni hana pengine pa kukata rufaa. Hana pa kukimbilia, wala pa kupinga. Mahakama imeamua anyongwe hadi afe. Jaji Stellah Mugasha amegonga nyundo. Itz over.
Hawezi kukata rufaa tena kwa sababu hukumu ya leo ni review ya hukumu iliyotolewa na mahakama hiyo September 16, 2016, ambapo alihukumiwa kunyongwa hadi kufa na jopo la majaji watatu wakiongozwa na Jaji Benard Luanda.
Itakumbukwa kwamba Bageni alikuwa Mkuu wa Upelelezi wilaya ya Kinondoni. Mwaka 2006 yeye na wenzake wakiongozwa na aliyekuwa Kaimu RPC Dar, Abdalah Zombe, walituhumiwa kupanga njama za kuwauwa wafanyabiashara watatu wa Morogoro.
Zombe anadaiwa ndiye aliyeongoza wenzie kwenye mpango huo, baada ya kujulishwa kuwa wana madini na fedha kiasi cha shilingi milioni 200.
Walikamata gari waliyokuwa wamekodi. Wakamuongoza dereva hadi msitu wa Mabwepande, Kinondoni, Dar es Salaam. Wakapora madini pamoja na fedha zote walizokuwa nazo. Kisha wakawafunga vitambaa vyeusi usoni na pingu mikononi. Kisha wakawapiga risasi za kisogoni na kuwauwa wote akiwemo dereva wa taxi waliyemkodisha.
Kesho yake Zombe akaita media na kusema wameua majambazi yaliyokua yanarushiana risasi na Polisi. Rais Kikwete akaunda tume ya Jaji Kipenka kuchunguza. Ikabainika hawakuwa majambazi. Kilichouma zaidi walikuwa ndugu wa familia moja. Mama mmoja alipoteza wanae watatu kwa tamaa za polisi.
Zombe alifanikiwa “kuchomoka” kwenye kesi hii baada ya kusota rumande kwa miaka kadhaa. Lakini Bageni alipatikana na hatia akahukumiwa kunyongwa. Akakata rufaa ikafeli, akaomba review ya kesi, na rulling imesomwa leo kuwa ANYONGWE HADI KUFA.
Waliomtuma hawapo nae Segerea, wala hawatanyongwa pamoja nae. Atanyongwa peke yake. Wanaohangaika nae saivi angalau kumfariji ni familia yake. Zombe hayupo, OCD wake hayupo hata IGP wa wakati huo hayupo. Ni yeye mwenyewe, na atanyongwa mwenyewe.
Hii iwe fundisho kwa wote wanaotumwa kuteka, kuua na kupoteza watu. Ipo siku utajikuta peke yako. Anayekutuma hatakuwepo. Utasimama wewe mwenyewe kutoa hesabu ya maovu yako. Kama si hapa duniani basi hata mbinguni, lakini ipo siku utalipa.
Kama ambavyo wema ni mbegu, na ubaya pia ni mbegu. Humea, hukomaa, na ni lazima UVUNE.!