Picha ya pamoja ni Kamati ya kudumu ya Bunge ya Huduma na Maendeleo ya Jamii mara baada ya kufanya ziara katika Tume ya Nguvu za Atomiki Tanzania, na kujionea shughuli mbalimbali zinazotekelezwa
KAMATI YA KUDUMU YA BUNGE HUDUMA NA MAENDELEO YA WATEMBELEA (TAEC) KUONA MRADI WA MAABARA TENGAMANO AMBAO UMEKAMILIKA KWA 94%
Na Vero Ignatus,Arusha
Kamati
ya kudumu ya Bunge ya Huduma na Maendeleo ya Jamii na imefanya ziara
katika Tume ya Nguvu za Atomiki Tanzania, na kuangalia utekelezaji wa
mradi na.6352 kuhusu ujenzi wa maabara tengamano, ambayo iliingia
mkataba na (TBA) kwaajili ya ujenzi huo awamu ya kwanza uliokuwa na
kiasi cha fedha bilioni 2.3 hadi kukamilika kwake
Akisoma taarifa ya utekelezaji huo leo katika makao makuu ya TAEC mkoani Arusha Mkurugenzi mkuu wa Prof.Lazaro Busagala amesema
kuwa, ujenzi huo ulihusisha maabara kupima viali kwenye sampuli,viwango
vya mionzi kwa wafanyakazi kwenye mazingira ya mionzi,uhakiki wa vifaa
vya kukagua mionzi,kupima vyanzo vya ionzi kenye mwili wa
binadamu,pamoja na kutoa mafunzo ya ulinzi na usalama wa vyanzo vya
mionzi.
Prof. Busagala
alisema kuwa awamu ya pili ya ujenzi wa maabara TAEC iliingia mkataba
na Li Jun Development Construction CO.LTD 2019 mkataba wa miaka 3,
ambapo una thamani ya bil.10.4,na kusema kuwa ujenzi rasmi changamano
ulianza 23sep 2019,hadi kufikia 09 machi 2022 ujenzi huo ulikuwa
umefikia 94%ambapo upo mbele kwa miezi mitatu
”Ujenzi
huo unahusisha maabara ya kupima mionzi ya alfa ,kupima mionzi Beta,ya
kupimia mionzi ya Gama ,kupima mionzi ya kwenye damu,viwango vya metali
kwenye sampuli,kutengeneza vifaa vya mionzi ,uandaaji wa sampuli na
kemikali,pamoja na maabaa ya kufanyia matengenezo ya vyanzo vya mionzi
na uchunguzi wa nyuklia.
Akichangia
katika majadiliano baada ya kufanya ziara ya kutembelea mradi huo
Mwenyekiti wa Kamati ya kudumu ya Bunge na Huduma ya Maendeleo ya jamii Aloyce John Kamamba ,ameipongeza TAEC kwa kutekeleza mradi huo kwani ni mzuri na unaridhisha na pesa zimetenda kazi iliyokusudiwa
Kamamba ameishauri
Tume hiyo kupitia Katibu wa kamati ya kudumu ya Bunge na Huduma ya
Maendeleo ya Jamii, kuandaa muda wa kutosha ili wabunge waweze kufahamu
kazi zinazofanywa na Taasisi hiyo, pamoja na changamoto zinazowakabili
kwani taarifa zinaonyesha kuwa hadi sasa vipo vituo 1200 ila kwa mwaka
ni vituo 650 tu vinafikiwa
Nae Mjumbe wa Kamati hiyo Mbunge wa Vyuo Vikuu Dkt.Pauline Nahato amesema
kuwa tume hiyo imeanzishwa mwaka 2003 ,ila yeye leo ndio anaifahamu
hivyo,amesema ipo haja ya wao kuhakikisha kuwa wanaitangaza ili watu
waifahamu, pamoja na utendaji kazi wake kwani ni wazi kuwa haifahamiki
kwa watu wengi
”2003
nilikuwa mbali sana unaweza kuona mimi leo ni kingozi na ndio naifahamu
Tume tena kwa uchache jamani,hebu wekeni mpango mkakati wa kujitangaza
ili jamii na Taasisi mbalimbali ziwafahamu kwani utendaji kazi wenu ni
mkubwa ila hamfahamiki jamani”alisema Nahato
Kwa upande wake mbunge wa Viti Maalum kutoka Lindi Tekla Ungele alisema
kuwa kwa upande wa kusini mwa nchi kuna mabaki ya vyuma vya silaha za
kivita ambayo yalikuwa yanatumiwa na wapigania uhuru wa nchi,hivyo
ameiomba TAEC kufanya mchakato wa kuweza kwenda kuviondoa kwani
vinaonekana ili visilete madhara kwa wananchi
Bila
shaka kwenye hizo zana zilizokuwa zinatumika kwaajili ya kupigania
uhuru sidhani kama hakuna vyenye mionzi,hivyo basi tunaiomba tume ipange
mkakati wa kwenda na kuona namna ambayo inaweza kuviondoa au namna
ambayo wanijua wao isijeleta madhara kwa jamii”alisema Ungele
Nae Waziri wa Elimu Sayansi na Teknolojia Prof.Adolf Mkenda ameishukuru
kwa dhati Kamati ya kudumu ya Bunge na Maendeleo ya Jamii ,kwa
kutembelea katika Tume ya Nguvu za Atomiki na kujionea kile
kinachoendelea pamoja na utekelezaji wa miradi mbalimbali.
Mkenda amesema ni matarajio ya Taasisi kuwa serikali itaendelea kuiwezesha kufikia malengo yake kwa manufaa ya jamii ya watanzania
Tume
ya Nguvu za Atomic Tanzania inatekeleza majukumu yake chini ya wizara
ya Elimu Sayansi na Teknolojia ,ilianzishwa 2003 kwa sheria no 7 ,lengo
la kuanzishwa ni kusimamia,kudhibiti na kuhamasisha matumizi salama ya
teknolojia ya nyuklia nchini,kulinda afya ya wafanyakazi,wagonjwa na
wananchi kwa ujumla.
Nae Mbunge kutoka Mwanakwerekwe Kasim Hassan Haji ameishauri wizara ya Elimu sayansi na Teknolojia kupitia waziri Prof.Adolf Mkenda kuangalia katika mitaala ya wanafunzi kuanzia shule za msingi hadi vyuo vikuu namna ambayo wanaweza kuweka somo la matumizi sahihi ya mionzi na madhara yake ili waweze kuifahamu kwa upana zaidi
”Nasema hivyo kwasababau ni kweli Tume hii ya inafanya kazi kubwa ni vyema jamii ikaifahamu kwa mapana zaidi hivyo jikiteni pia kwa kutumia vyombo vya habari zaidi na kualika taasisi mbalimbali kuja kuwatembelea mtajenga wigo mpana zaidi”Alisema Haji
Mwisho
Reply
Forward