Kampuni ya kibo seed ltd yatuhumiwa kutapeli mil 404 kwa wakulima 4 njombe


NJOMBE
Wazee wanne ambao ni wakulima wa mahindi katika kijiji cha Mavanga wilayani Ludewa mkoani Njombe pamoja na vijiji vya Madaba na Mahanje vilivyopo wilayani Madaba wilayani Ruvuma wamemuomba rais wa jamhuri ya muungano wa Tanzania Dr John Pombe Magufuli kuwasaidia kupata stahiki zao za mauzo ya mahindi ya mbegu yenye thamani ya mil 407 katika kampuni ya KIBO SEED COMPANY LTD ambayo waliuzia kampuni hiyo 2016.
Wakulima hao wamesema wapo hatarini kupoteza haki yao ambayo baada ya mauziano waliahidiwa kulipwa kwa awamu na kampuni hiyo jambo ambalo limekuwa tofauti hivi sasa kwa kuwa uongozi wa kampuni hiyo umekana kudaiwa fedha ya mauzo ya mbegu za mahindi na wakulima hao.
Wakifafanua sababu ya kuomba rais kuingilia kati madai yao ya kipindi kirefu wakulima hao akiwemo Vitus Chaula, Stephano Mahundi, Eletel Mlelwa na Deusdedith Hunja wanasema wamelazimika kutuma ujumbe huo kwa rais Magufuli kwasababu wamefanya kila jitihada za kupata fedha yao lakini zimegonga mwamba.
Wakulima hao wamesema wanakila kielelezo na mikataba inayothibitisha kuidai kampuni hiyo yenye makazi yake jijini Arusha lakini wanashangazwa kuona mkurugenzi anakanusha kudaiwa fedha hizo ili hali walisainiana mkataba wa makabidhiano ya mauziano ya mbegu hizo za mahindi 2016 na kukubaliana kulipana fedha baada ya siku 15 jambo ambalo limekiukwa na uongozi wa kampuni hiyo.
Katika hatua nyingine wakulima hao wameeleza namna kukikukwa kwa mkataba wa malipo hayo kulivyo athiri maisha yao ambapo wamelazimika kuuza mali zao na wengine kushindwa kusomesha watoto huku pia wakilalamikia kuahilishwa mara kwa mara kwa kesi yao madai kwa zaidi ya miaka miwili jambo ambalo linazidi kuwapa mazingira magumu katika familia zao.
Mtandao wa fullshangwe umezungumza kwa njia ya simu na mkurugenzi wa kampuni ya KIBO SEED ltd iliyopo mkoani Arusha Fransis Chege ambaye anabaki na msimamo wake kwamba kampuni haidaiwi fedha yeyote na wakulima hao ambao awali walikuwa wakifanya nao biashara ya mbegu za mahindi na kudai kwamba fedha inayotajwa na wakulima haina ukweli kwasababu mzigo uliochukuliwa mwaka 2016 ulirudishwa kwa wakulima kwa kuwa haukukithi vigezo vya mbegu bora.
Utaratibu wa kurejesha kwa wakulima mbegu zilizochukuliwa haukufanyika kienyeji kwasababu mbegu zilizochukuliwa na kampuni zilifanyiwa utafiti kwa kipindi cha mizezi mitano na taasisi ya uthibiti wa mbegu TOSCI na kisha kutoka na ripoti ya kwamba hazina ubora hivyo kutokana ripoti hiyo kampuni akarudisha mbegu zote kwa wakulima.
“Wakulima walirudishiwa mbegu zote walizoleta kwenye kampuni baada ya kubainika zimekosa ubora na kisha kuamua kuziuza kwa wazalishaji wa unga mjini Makambako”anasema mkurugenzi wa KIBO Frank Chege.
Baada ya majibu hayo wakulima hao wanakanusha kurejeshewa mbegu hizo kwa madai ya kwamba tangu zichukuliwe hazijawahi kurudishwa kwa wakulima na kudai kwamba kuna kila hali ambayo inaonyesha mazao yao yameuzwa na kampuni hiyo na fedha kuliwa .