Kampuni ya pembejeo za kilimo yara yawakumbuka mawakala wa pembejeo za kilimo mapambano ya ugonjwa wa covid 19

Meneja wa Kanda ya Kaskazini wa kampuni ya Uuzaji wa Pembejeo za Kilimo ya YARA Philipo Mwakipesile akiongea kwenye hafla ya kuwakabidhi mawakala wa uuzaji wa pembejeo za Kilimo mkoa wa Arusha vifaa vya kujikinga na maambukizi ya Ugonjwa wa Covid 19  katika hafla iliyofanyika kwenye hotel ya Kibo Palace jijini Arusha

Mgeni Rasmi Kaimu Katibu Tawala Mkoa wa Arusha David Lyamongi akiwasili katika Hafla hiyo ya kuwakabidhi mawakala wa Pembejeo za Kilimo vifaa vya kujikinga na maambukizi ya ugonjwa wa Covid 19 iliyofanyika kwenye ukumbi wa hotel ya Kibo Palace jijini Arusha

Kaimu Katibu Tawala mkoa wa Arusha David Lyamongi akiongea na mawakala kabla ya kuwakabidhi vitakasa mikoni sabuni na ndoo ya kuoshea mikono iliyotolewa na Kampuni ya uuzaji wa pembejeo ya YARA katika hafla iliyofanyika kwenye Hotel ya kitalii ya Kibo Palace jijini Arusha

Mganga mkuu wa mkoa wa Arusha Dkt.Wilson Sichalwe akitoa taarifa ya kimkoa ya ugonjwa wa Covid 19 na kuwataka watanzania na wakazi wa mkoa wa Arusha kuendelea kutoa elimu zaidi ikiwa ni pamoja na kuchukuwa hatua na maelekezo ya wataalamu kutozalisha maambukizi mapya ya ugonjwa wa homa kali ya mapafu covid 19

Mgeni Rasmi wa hafla ya kukawakabidhi Mawakala wa Pembejeo mkoa wa Arusha vifaa vya kujikinga na maambukizi ya ugonjwa wa homa kali ya mapafu inayosababishwa na virusi vya Corona akiosha mikono kwa kutumia maji tiririka na sabuni  akiangaliwa na Mganga mkuu wa mkoa wa Arusha Wison Sichalwe na Meneja wa kanda ya kaskazini wa Kampuni ya YARA Philipo Mwakipesile 

Picha Juu na chini ni Mkurugenzi wa duka la Pembejeo za kilimo la Beartice Agrovet akikabidhiwa vifaa vya kujikinga na maambukizi ya ugonjwa wa Covid 19 huku akitoa ishara za salamu kwa kipindi hicho cha Ugonjwa wa covid 19  ikiwa ni kufuata maelekezo ya wataalamu wa Afya kwenye hafla ya kuwakabidhi vifaa mawakala hao wa pembejeo  mkoa wa Arusha

Arusha
Watanzania wameaswa kuendelea kuchukua hatua na kufuata
maelekezo ya wataalamu wa Afya sanjari na kuendelea kutoa elimu ya kuepuka
maambukizi mapya ya ugonjwa wa covid 19.
Kauli hiyo imetolewa na Kaimu Katibu tawala wa mkoa wa
Arusha David Lyamongi wakati akikabidhi vifaa vya kujikinga na maambukizi ya
Ugonjwa wa Covid 19 kwa mawakala wa uuzaji wa Pembejeo mkoani humo kwenye hafla
iliyofanyika jijini Arusha.
Alisema kuwa kipindi hicho maambukizi ya ugonjwa huo yakiwa
yamepungua nchini elimu juu ya janga hilo inatakiwa kuendelea kutolewa ili
kuweza kuutokomeza kabisa ugonjwa huo nchini na kuwashukuru kampuni ya YARA
kuona umuhimu wa kuwakumbuka wateja wao wakiwamo wakulima.
“Sote ni mashahidi wakulima ni kada muhimu sana ndio maana
mh.Rais wetu aliliona hilo na kuacha kutufungia ndani ilituendelee na
uzalishaji kipinchi chote cha janga la ugonjwa huu hivyo tuonyeshe kuunga mkono
kwa kufuata maelekezo ya wataalamu wa Afya ili kuweza kuutokomeza nchini mwetu”
Awali Mganga mkuu wa mkoa wa Arusha Dkt.Wilson Sichalwe
alisema kuwa elimu zaidi inahitajika kwa wananchi sanjari na utoaji vifaa hivyo
ujumbe uendelee kutolewa ilikuendeleza mapambano ya kuuondoa hapa nchini.
Alisema mkoa umejipanga kuhakikisha unaendelea kutoa elimu
kwa umma na kuendelea kuona hakuna maambukizi mapya yanayoweza kutokea kwa
kufuatlia na kuchukuwa hatua ikiwemo elimu kwa umma kama walivyokuwa wakifanya
awali.
Nae Meneja wa Kampuni ya uuzaji na uzalishaji wa Pembejeo za
kilimo YARA Kanda ya kaskazini Philipo Mwakipesile alisema kuwa kampuni hiyo
imetoa msaada huo wenye thamani ya million 82 kwa mawakala wa pembejeo wa
ukanda huu wa kaskazini na walianza na Uknda wa kusini na watamalizia ukanda wa
ziwa.
Alisema lengo la utoaji wa vifaa hivyo vya kujikinga na
maambukizi ya ugonjwa wa homa kali ya mapafu kwa mawakala ni kuunga mkoano
serikali kuhakikisha inaendelea kupunguza maambukizi mapya na kuona ugonjwa huo
unaondoka ndani ya jamii ya watanzania na duniani kwa ujumla kwa kuwa
umechukuwa nmaelfu ya wenzetu duniani kote hivyo sekta ya kilimo ni muhimili
mkubwa wa uchumi hapa nchini ndio maana wakaona waanze nayo.

Mwisho