Ajali ya magari, bajaji yaua na majeruhi jijini mbeya

AJALI YA GARI KUGONGA GARI NA KISHA KUGONGA BAJAJI KUSABABISHA KIFO NA MAJERUHI.


Mnamo tarehe 08.06.2020 majira ya saa 10:00 Asubuhi huko eneo la Nzovwe, Kata ya Itende, Tarafa ya Iyunga, Jijini Mbeya katika barabara ya Mbeya – Tunduma, Gari lori Tanker la Mafuta lenye namba za usajili T.198 BRP Tela namba T.329 BHS aina ya Benz mali ya KISMA TRANS likiendeshwa na SAID JOKA likitokea Dar es Salaam kuelekea Zambia liligonga Gari T.624 DCY aina ya Toyota Hiace ikiendeshwa na PETER VALENTINO MGAYA na kwenda kugonga Bajaji MC.948 CNV aina ya TVS KING ikiendeshwa na MAJID JUMA [21] Mkazi wa Iyunga na kusababisha kifo papo hapo kwa Dereva wa Toyota Hiace aitwaye PETER VALENTINO MGAYA.


Aidha katika ajali hiyo watu watatu waliokuwa kwenye Bajaji wamejeruhiwa ambao ni:-

    JAPHET MAFRENI [52]
    INANI MWAIGAGA [23]

    MAJID JUMA [21] Dereva wa Bajaji.