Mkurugenzi Halmashauri ya wilaya ya Mbinga Juma H.Juma |
Joyce Joliga,Mbinga
Afisa Elimu kata ya Kingosera iliyopo Halmashauri ya wilaya ya Mbinga , Mwimbira Gallus amesema kata yake imefanikiwa kudhibiti vitendo vya unyanyasaji watoto kingono kutokana na kutoa elimu kwa jamii ili kumlinda mtoto asiumizwe.
Akizungumza na Blog hii Gallus alisema ,Vitendo vya unyanyasaji kwenye kata hiyo hakuna kutokana na elimu ambayo imekuwa ikitolewa mara kwa mara na wataalamu wa halmashauri ya wilaya ya Mbinga,kwa kushirikiana na walimu ili kumlinda mtoto na mafedhuli na kumweka kwenye mazingira salama.
“Tunashukuru Mungu kwenye kata yangu sina kesi za Ulawiti wala ubakaji watoto kwani tumekuwa tukitoa elimu kwa kushirikiana na Dawati la jinsia, Walimu na wataalamu wa Halmashauri ,na tumefanikiwa kudhibiti vitendo hivyo na kuwaweka watoto kwenye ulinzi na usalama,alisema.
Aidha ameitaka jamii kuendelea kuwalinda na kuwathamini watoto kwani nao wanahaki ya kuheshimiwa na kulindwa kama watu wengine.
Naye Mwalimu Mkuu wa shule ya Msingi Halale Gaudence Luambano alisema ,wameweka mkakati kuhakikisha watoto wanasoma bila kulata matatizo ambapo wamewaeleza namna ya kujilinda na hakuna vitendo hivyo katika shule hiyo.