Waandamanaji wanaopinga Brexit – Uingereza kujitoa katika Muungano wa Ulaya walikusanyika huko Whitehall, karibu na Downing Street |
Others gathered outside Parliament late into the evening |
Hatua hiyo ilichangia kuzuka maandamano kote nchini, kesi iliowasilishwa dhidi ya hatua hiyo na waraka uliosainiwa na zaidi ya watu milioni moja kupinga hatua hiyo.
Serikali imesema kuistishwa kwa wiki tano kwa vikao vya bunge mwezi Septemba na Oktoba kutaruhusu muda wa kutosha kujadili Brexit.
lakini wakosoaji wanasema ni hatua “isio ya kidemokrasi ” kuwazuia wabunge kupinga brexit bila ya mpangilio.
Waziri Michael Gove ameiambia BBC kwamba kusitishwa huko kwa bunge kulikoidhinishwa na Malkia siku ya Jumatano ‘bila shaka sio’ hatua ya kisiasa kuzuia upinzani kwa hatua ya Uingereza kujitoa katika Muungano wa Ulaya pasi kuwepo mpangilio.
Ameeleza kwamba kutakuwa na “muda mwingi” kujadili Brexit kabla ya muda ulioorodheshwa wa kuondoka Oktoba 31.
Hapo jana Jumatano Bwana Johnson alisema hotuba ya Malkia itatolewa baada ya kusitishwa kwa vikao vya bunge, ifikapo Oktoba 14 kueleza ‘ajenda yake ya kusisimua’.
Amesema hataki kusubiti maka baada ya Brexit “kabla ya kuendelea na mipangilio ya kuisogeza nchi hii mbele”. Haki miliki ya picha AFP Image caption Waandamanaji wanaopinga Brexit – Uingereza kujitoa katika Muungano wa Ulaya walikusanyika huko Whitehall, karibu na Downing Street
Kiongozi wa bunge Jacob Rees-Mogg, aliyekuwa katika mkutano na Malkia amesema vikao hivi vya bunge vilikuwa virefu kuwahi kushuhudia katika takriban miaka 400, kwahivyo ni sawa kusitishwa na kuanza kikao kipya.
Kiongozi wa chama cha Leba Jeremy Corbyn ameitaja hatua hiyo kama “pigo na unyakuzi kwa demokrasia yetu” ili kulazimisha Brexit bila ya mpangilio kwa kuwaacha wabunge pasi kuwana muda w akutosha kupasisha sheria bungeni. Aliahidi kujaribu kuisitisha hatua hiyo ya kusitishwa bunge.
Na mwanaharakati anayepinga Brexit Gina Miller – aliyewahi kushinda kesi dhidi ya mawaziri kuhusu kipengee cha ‘Article 50’ – amewasilisha ombi la kuikagua sheria dhidi ya uamuzi huo wa Johnson.
Waziri mkuu huyo anasema anataka kuondoka katika Umoja wa Ulaya mwishoni mwa Oktoba huku kukiwepo na mpangilio lakini yuko radhi kuondoka pasi kuwepo mapngilio huo kuliko kuikosa tarehe ya mwisho. Haki miliki ya picha Getty Images Image caption Others gathered outside Parliament late into the evening
Hisia imekuwaje kwingine?
Jumatano jioni waandamanaji walikusanyika Westminster wakipiga kelele wakisema “sitisha mapinduzi” huku wakibeba mabango ya kupinga kujitoa katika Umoja wa Ulaya na benderea za Muungano huo.
Maandamano haoy – yalioandaliwa saa chache awali – yalianza nje ya makao ya bunge kabla ya kusambaa kuelekea huko Downing Street.
Katika eneo hilo, mandishi wa BBC aliitaja hali kuwa ya amani na ya kuchangamsha.
Waandamanji kadhaa waliozungumza na BBC waliashiria kwamba huu ni mwanzo tu wa ukosefu wa utulivu, kukiwa kumepangwa maandamano zaiid mwishoni mwa juma.
Wakati huo huo mswada wa kielektroniki katika matndao wa serikali unaotaka bunge lisisitishwe ulifanikiwa kupokea saini za watu zaidi ya milioni moja katika muda wa chini ya siku moja.
Vipi kuhusu kesi iliowasilishwa?
Watu kadhaa wakuu, akiwemo aliyekuwa waziri mkuu John Major, waliwahi kutishia katika siku za nyuma kwenda mahakamani kusitisha hatua ya Johnson iwapo atalisitisha bunge ili kuwasilisha Brexit pasi kuwepo mpangilio.
Baada ya tangazo hilo, Sir John alisema “hakuwa na shaka” lengo la Johnson lilikuwa ni “kuvuka bunge lililo na uhuru, linalopinga sera zake kuhusu Brexit”, na kwamba ataendelea kupata ushauri wa kisheria. Haki miliki ya picha Getty Images
Mahakama kuu ya kiraia Scotland tayari inafikiria kuwasilisha kesi kupinga kusitishwa bunge, itakayoongozwa na msemaji wa kisheria wa SNP, Joanna Cherry.
haiwezekani kuwasilisha kesi ya kisheria dhidi ya hatua aliyochukua Malkia inayotokana na mamlaka yake binafsi.
Lakini Bi Miller – ambaye awali alishinda kesi dhidi ya mawaziri kuuus kifungu cha sheria Article 50 kinachoruhusu kucheleweshwa kuidhinishwa kwa Brexit ameiambia BBC: “Iwapo nia ya kutumia hatua ya kuistishwa bunge na athari yake ni kuwa inazuia uhuru wa bunge, basi tunaamini kwamba ni kinyume cha sheria na kinyume na katiba.”
Mwandishi wa masuala ya sheria wa BBC Clive Coleman ansema iwapo wanasheria wa Bi Millerwanaweza kubaini kwamba nia ya kuistishwa bunge ni “kutatiza shughuli za demokrasia za bunge”, basi ” hilo litang’ang’aniwa “.
Kwa kawaida bunge husitishwa – kwa kipindi kifupi kabla ya kikao kipya kuanza katika muda ambao hakuna mijadala inayofanyika wala kura kupigwa.
Haina tofuati na hatua ya ‘kulivunja’ bunge, ambapo wabunge wote hupoteza viti vyao ili kukampeni katika uchaguzi mkuu.
Hatua hi ikiidhinishwa bunge litafungwa kwa siku 23 za kazi na wabunge hawawezi kuizuia.