Mwandishi wetu, Loliondo
Arusha. Matumizi ya maarifa ya asili katika uhifadhi wa misitu, vyanzo vya maji na Mazingira umesaidia jamii ya wafugaji Kata ya Enguserosambu kutoathirika na mabadiliko ya tabia nchi.
Wakizungumza na waandishi wa habari waliofika katika Kata hiyo, ,kupitia mradi wa uhifadhi Mazingira kwa maarifa asilia ambao unatekelezwa na taasisi ya Usaidizi wa jamii za Pembezoni (MAIPAC) kwa kishirikiana na taasisi ya CILAO katika mradi unaodhaminiwa na shirika la maendeleo la umoja wa mataifa(UNDP) kupitia program ya miradi midogo na kuratibiwa na Jumuiko la maliasili Tanzania (TNRF) baadhi ya viongozi wa Mila na serikali wameeleza matumizi ya maarifa ya asili yamekuwa na ufanisi mkubwa.
viongozi wa hao wamila na serikali katika Kata ya Enguserosambu,walieleza kuwa na sheria kali imesababisha, mazingira na kufanya kata hiyo, kuwa na msitu mkubwa wa asili wenye hekta 14,700.
Kiongozi wa Mila Parmitoro Pumbun alisema wamekuwa na sheria ya Mila kutoza faini ya Ndama jike, kulaaniwa ama kunyang’anywa mke kwa ambao watabainika kukata Miti ama kuharibu Mazingira.
Laigwanani Pumban alisema faini hizo, zimesababisha Kata yao kuwa ya mfano katika utunzwaji wa mazingira kwa kutumia maarifa ya asili.
Katibu wa bodi ya msitu wa Enguserosambu, Marko Tarash alisema msitu wao umekuwa na faida kubwa kwa jamii kwani, wana uhakika kupata malisho ya mifugo mwaka mzima,kupata dawa za asili,matunda,maji na Kuni za kupikia.
Tarash alisema msitu huo unaundwa na vijiji vinne ambavyo ni Enguserosambu,Ng’arwa,Orkiu na Naan.
Afisa Mtendaji Kijiji cha Enguserosambu Duni Mollel alisema uwepo Sheria za Mila umesaidia sana uhifadhi kwani Wananchi wanaziheshimu zaidi.
“Ingawa tuna sheria ndogondogo za serikali kuhifadhi misitu na vyanzo vya maji lakini Sheria za Mila ndizo zinaogopwa zaidi na Wananchi wa huku”alisema
Mwalimu Edward Sasi wa shule ya msingi Enguserosambu alisema licha ya kuwepo elimu ya kisayansi lakini nao wao katika shule wamekuwa wakisisitiza wanafunzi kuzingatia elimu ya asili katika uhifadhi.
“Vijana wanajua misitu ndio maisha Yao kwani wanategemea mifugo Sasa ikiathirika na kukosa malisho na maji wao ndio wanapata shida Sasa wanajituma kutunza Mazingira na vyanzo vya maji”alisema
Mwanafuzi Regina Zakayo alisema utunzwaji wa misitu umekuwa na faida kubwa hata kwao kwani kwenye msitu huo pia wanapata maji na dawa sa asili ambazo wanaotumia kutibu magonjwa mbalimbali.